Je, huu ndio mtindo mpya wa utendaji kazi wa awamu ya kutumia vyombo vya habari hata kwa vitu visivyo na ulazima?

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Nimependa tu kueleweshwa kwa kina maana nimekuwa nikijiuliza sipati majibu. Imekuwa ni kawaida kila kiongozi katika awamu hii ya tano kutumia vyombo vya habari kila kuitwapo leo. Matamko yote ya kutumbua watu na matukio mbalimbali viongozi hawa wamejisogeza kwenye kamera za waandishi wa habari.

Mbaya zaidi ni pale kunapokuwa na mambo ya siri, confidential issues yanayotakiwa yafanyike kwa usiri mkubwa, mfano mdogo ni huu wa spika wa bunge kutoa wito wa kumtaka CAG kupitia vyombo vya habari badala ya kumwandikia barua ya wito.

Je huu ndio mtindo mpya wa utendaji kazi katika awamu hii ya tano.
 
Kwani huyo CAG malalamiko yake kwa bunge aliyatoa kwa barua?

Ngoja wararuane mimi zangu popcorn tu.
 
Kwani kuna shida?

Hapana ila kuna dashi
057884c793b30126259c424ea5e0c8bb.jpg

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwani huyo CAG malalamiko yake kwa bunge aliyatoa kwa barua?

Ngoja wararuane mimi zangu popcorn tu.

Nani alikuambia CAG alikuwa analalamika? upotoshaji ni mwingi sana. CAG alikuwa anahojiwa alipokuwa anajibu swali ndio akaeleza hali halisi ya bunge letu kuwa ni dhaifu kuisimamia serikali
 
Nimependa tu kueleweshwa kwa kina maana nimekuwa nikijiuliza sipati majibu. Imekuwa ni kawaida kila kiongozi katika awamu hii ya tano kutumia vyombo vya habari kila kuitwapo leo. Matamko yote ya kutumbua watu na matukio mbalimbali viongozi hawa wamejisogeza kwenye kamera za waandishi wa habari.

Mbaya zaidi ni pale kunapokuwa na mambo ya siri, confidential issues yanayotakiwa yafanyike kwa usiri mkubwa, mfano mdogo ni huu wa spika wa bunge kutoa wito wa kumtaka CAG kupitia vyombo vya habari badala ya kumwandikia barua ya wito.

Je huu ndio mtindo mpya wa utendaji kazi katika awamu hii ya tano.
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums
P
 
Back
Top Bottom