Je, hukumu za mahakama zetu zinaendana na uhalisia wa makosa?

Navoyne

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
874
373
Habari zenu,

Katika pita pita zangu za magazetini huwa na soma habari za yalijiri kwenye mahakama zetu, mara nyingi nakutana na habari nyingi ambazo hukumu zake nahisi kama ni kukomoa na sio tena kurekebisha hawa wakosaji ili waweze kurudi tena kwenye jamii kama watu walioelimika na kuitumikia jamii upya.

Pili, kuna hukumu nyingine huwa na mashaka kama zina tekelezeka,hasa hizi za kifungo na faini je nikweli mahakama zetu zinapokea hizi faini?? na kama hawapokei kwanini wanaendelea kutoa hizi faini. Mfano wa hukumu ninazozungumzia ni hizi "Mahakama ya hakimu mkazi Tanga imemhukumu kwenda jela miaka 25 na faini ya shilingi bilioni 4 mfanya biashara Michael Kijangwa baada ya kupatikana na kosa la kusafirisha meno ya tembo yenye uzito wa tani elfu 5." , habari kamili

Naomba tujadili je hizi hukumu zinaendana na uhalisia wa makosa na pia hukumu na jela zetu zinalenga kufundisha au kukomoa?
 
Hukumu zote hutokana na Sheria Mkuu. Sheria huweka sifa za kosa na adhabu zake. Kimsingi, Sheria huweka adhabu ndogo kabisa na kubwa kabisa. Huweka adhabu za kifungo, faini au zote kwa pamoja. Ni uamuzi wa Mahakama, kwa kuzingatia yaliyosemwa na kuwasilishwa mahakamani, kutoa adhabu fulani.
 
Sasa mfano mtuhumiwa anafungwa miaka 25 na faini ya billion 4 na yeye hana hizo pesa inakuaje??
 
Sasa mfano mtuhumiwa anafungwa miaka 25 na faini ya billion 4 na yeye hana hizo pesa inakuaje??
Ziko njia za kutekeleza hukumu ya mahakama. Kama hana hata mali za kukamatwa na kupigwa mnada, mhusika atatamkwa kuwa amefirisika. Hatakopa wala kukopesha katika maisha yake.
 
Ziko njia za kutekeleza hukumu ya mahakama. Kama hana hata mali za kukamatwa na kupigwa mnada, mhusika atatamkwa kuwa amefirisika. Hatakopa wala kukopesha katika maisha yake.
Wewe unaamini hizi faini huwazinapatikana?, halafu hizi sheria zetu naona kama kipindi hiki zimebadilika sana mtu ametukana tu anaambiwa alipe millioni 7 nakumbuka zamani ilikuwa elfu 30 na kama umempiga unalipa matibabu na kiasi kidogo cha usumbufu.
 
9aa6f1b80c09ebcc08a1b364ad15178d.jpg
 
Wewe unaamini hizi faini huwazinapatikana?, halafu hizi sheria zetu naona kama kipindi hiki zimebadilika sana mtu ametukana tu anaambiwa alipe millioni 7 nakumbuka zamani ilikuwa elfu 30 na kama umempiga unalipa matibabu na kiasi kidogo cha usumbufu.
Rejea mchango wangu wa awali kabla ya huu uliounukuu
 
Rejea mchango wangu wa awali kabla ya huu uliounukuu
Nimeusoma ila tatizo mahakama zetu zinaonekana hukumu zake zipo tofauti sana yaani naona ni kama kila hakimu au jaji anafafanua sheria anavyojua yeye ndio maana raia wengi wanaona kuna "double standard " kwenye hukumu.
 
Back
Top Bottom