Je, hukumu ya Sabaya ina mtazamo gani juu ya kesi ya Mbowe?

Ngengemkenilomolomo

Senior Member
Mar 21, 2015
185
250
Wakuu kuhusu kilichotokea huko kwa kwa Sabaya ni kama mlivosikia, swali ni je hukumu hiyo imetolewa kama kuwafumba macho Watanzania ili itakapotolewa (mvua) hukumu kwa Mbowe ionekane kwamba imetenda haki?

Kwa hukumu hiyo ya Sabaya inaleta taswira gani kwa hukumu ijayo ya Mbowe?
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,718
2,000
Unajua ikoje? Iko hivi, ugaidi wa Mbowe ni kutaka kuwadhuru "viongozi" wa serkali; na kiongozi wa serikali anayetajwa kutaka kudhuriwa na "gaidi" Mbowe ni Ole Sabaya ambaye mahakama leo imeuthibitishia ulimwengu kwamba ni JAMBAZI LILILOKUBUHU na limekatiwa miaka 30 jela!

Sasa najiuliza, ugaidi wa Mbowe ulikuwa kulifanyia ugaidi jambazi tena jambazi lililotumia zana za moto? Jambazi lililojificha kwenye mwamvuli wa ukuu wa wilaya aka DC? Mbowe sio gaidi!
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,768
2,000
Hizi kesi mbili tofauti kabisa. Na uzuri ni kwamba, zote mwenendo mwenendo wa mashauri yake yanafanyika kwa uwazi na kila mtu kuona...

å Moja ya mhalifu wa kweli mwenye historia ya wazi na mbaya kabisa ya uhalifu - OLE LENGAI SABAYA NA WENZAKE.

å Ya upande wa pili, ni kesi ya KISIASA yenye malengo ya kisiasa kwa nia kuumiza na kukomoa isiyojengwa (not established) ktk msingi wa kisheria. Ni kesi ya mtu asiye na historia [rekodi] ya uhalifu popote, FREEMAN MBOWE NA WENZAKE
 

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
144,795
2,000
Una akili sana mkuu. Huyu boya katolewa kafara tu (jambo la kawaida katika siasa). Na hii inaweka mazingira mazuri sana kwa hiyo kesi nyingine ili huyo "gaidi" akija kupigwa mvua 40+ kusiwe na malalamiko. Yetu macho!
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
25,601
2,000
Dogo kafungwa sababu ya ujinga wake, na ndiyo maana DPP ambaye ndiye boss wa mashitaka yote nchini anayemwakilisha Rais hakuifuta kesi.

Dogo alionywa mara kibao na mabosi wa usalama awe makini akagoma sababu babake alimlinda...hakulidwa kwa kauli ya kisheria hapana bali alilindwa kwa kauli ya mdomoni ... sasa babake hayupo.... sheria imeruka naye kama mwewe.. mvua sate.

Kuhusu Mbowe na ugaidi na hukumu hii havina uhusiano...nachokiona mimi ni timu mwendazake waliomwaminisha maza kwamba wana ushahidi ulioshiba kuumbuka vibaya saana.

Hapa ndipo CCM watakapomjua Maza kwamba hatabiriki, yaani kama mvua za hapa dsm...inaweza nyesha manzese wafuriko wakati magomemi pakavuu.
 

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,416
2,000
Each case is treated on its own merit, there is no way one can draw a parallel between both criminal litigations.

Sabaya truly committed the offence and has been justly convicted by the court whereas in the Mbowe's context, the case is a fabricated one and without prima facie evidence.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
25,601
2,000
Kwa Sabaya kuna watu wameumizwa na wameumizwa

Kwa Mbowe hakuna aliyeumizwa wala kulalamika , watuhumiwa wameteswa na kuumizwa na polisi , na zaidi polisi kutuonyesha kuwa hawajui PGO ni nini
Its very low or rather shame to a Senior Police officer who doesn't even know the Police General Order procedures.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
14,930
2,000
Wakuu kuhusu kilichotokea huko kwa kwa sabaya ni kama mlivosikia,swali ni je hukumu hiyo imetolewa kama kuwafumba macho watanzania ili itakapo tolewa (mvua) hukumu kwa mbowe ionekane kwamba imetenda haki??
Kwa hukumu hyo ya sabaya inaleta taswira gan kwa hukumu ijayo ya mbowe?

Hukumu si gombesugu mjomba.

Kesi mbili ulizotaja hazihusiani zaidi ya kuwa sasa mfungwa aweza kuja kuwa shahidi wa nyingine.

Kimfungacho mtu ni ushahidi kwa mujibu wa sheria.

"Imethibitika pasi na shaka kuwa Sabaya na wenzake walivamia duka wakiwa na silaha, wakachukua mali na wakajeruhi pasipokuwa na uhalali wowote."

Baada ya hapo kifuatacho ni mazungumzo baada ya habari tu.

Kesi ya Mbowe inaingia je hapo sasa?
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,291
2,000
Papai na chungwa Ni tofauti japo yote Ni matunda. Mpaka Sasa hakuna dalili ama ushahidi dhahiri kwa vitendo vya kigaidi kutendeka ama kuandaliwa kutendeka na Mbowe na wenzake. Ilihali Upande wa Shauri Sabaya facts zilikiwa wazi hata kwa mtoto mdogo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom