Je, hotuba ya Rais ina uhusiano wowote na bajeti ya mwaka huu au itakuwa na uhusiano na bajeti ya mwakani?

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Sijaelewa kitu kimoja naomba mnifafanulie vizuri

1. Mapendekezo na aliyoyasema kuyafanya au kuyatekeleza je yana uhusiano na bajeti ya Mwaka huu au yatakuwa na uhusiano na bajeti ya mwakani.

Mfano Bima ya Afya kwa wote, maeneo tajwa kujenga barabara na hayakujadiliwa kwenye bajeti ya mwaka huu, Miradi ya maji na Elimu.

Endapo atakuwa ametaja vitu ambavyo atavitekeleza na kuanza kuvitekeleza mwaka huu hadi mwakani na tusema havikuwa kwenye bajeti ya mwaka huu fund allocation inakuwa ina reflect wapi na matumizi yake yanakuwa ni ya fedha za dharura au maana atakuwa ametumia pesa ambazo Bunge halija idhinisha.

Ufafanuzi naombeni kwa walio muelewa.
 
Ili kupata jibu hapo inabidi ujiulize je uwanja wa ndege wa Chato ulijengwa na bajeti iliyoidhinishwa na bunge gani? Matumizi mengi ya awamu Hii yanafanyika tuu bila kupata idhini ya bunge na hata bajeti zinazosomwa bungeni ni kama desturi tuu kwani nyingi huwa hazitekelezeki
 
Kama nakumbuka alisema kutokana na Ilani ya chama chake kilichompitisha kuwa raisi
Inaakisi bajeti kwa miaka yote ya kutekeleza Ilani ya chama
 
Kama nakumbuka alisema kutokana na Ilani ya chama chake kilichompitisha kuwa raisi
Inaakisi bajeti kwa miaka yote ya kutekeleza Ilani ya chama
Ladba tuseme ni ya bajeti ya mwakani maana ilani imetoka baada ya bajeti ya mwaka huu
 
Sio rahisi afanye yote aliyoyasema kwenye hotuba yake, lakini kwa yale machache atakayofanya, atachomoa pesa popote afanye atakavyo kama ambavyo amekuwa akifanya awamu yake ya kwanza, na hii ndio sababu mojawapo ya kuwaondoa kwa lazima wapinzani bungeni, now anajua hakuna atakayeuliza.

Huyo Gwajima kusema atahoji hajui anachoongea, atajikausha kimya, ukishamsifia mfalme huwezi kesho kugeuka umponde.
 
Mkuu kwa taarifa yako hata huu ujenzi wa SG haupo kwenye mpango wowote wa TANESCO, ambalo ndio shirika la umeme nchini. Kwa katiba yetu ukiw rais unaweza kufanya chochote bila kuguswa na yoyote.

Nadhani hata akina JK wanasikitika sana kuwa walikuwa na mamlaka ya kufanya chochote na mtu yoyote asikohoe. Katengeneza precidence mbaya sana, yoyote atakayekuwa rais wa nchi hii atafanya atakacho.
Hivi unajua tabia yake hii wanaiga wengine ambao ni ma rais watarajiwa ndani ya ccm mana yake anawafundisha la kufanya
 
ladba tuseme ni ya bajeti ya mwakani maana ilani imetoka baada ya bajeti ya mwaka huu
Uko sahihi hotuba hii ya Rais ni Dira na Mwelekeo wa nchi kwa miaka mitano ijayo hivyo utekelezaji wake unaanza mwaka 2021/2022 na hivyo bajeti hiyo itazingatia ilani ya uchaguzi 2020-2025 na ahadi za kwenye jukwaa la kampeni na viporo miradi inayoendelea.
 
Huyu jamaa hana vya budget wala nini

Na hakuna cha kumfanya

Inategemea ameamukaje
Tusifichane huo ndio ukweli hana bajeti plan kabisa kinachotoke akilinikwaeke hakipi muda wa kukichambua au kupata ushauri hatari sana kunasiku atawasha kibiriti kwenye eneo hatari ndipo tutalia na kusaga meno
 
Haujaelewa nini wakati awamu iliyopita alikuwa anatoa pesa za maendeleo nje ya bajeti, pesa yote siku hizi anayo yeye.
 
Back
Top Bottom