Mzukulu
JF-Expert Member
- Feb 14, 2020
- 1,401
- 2,631
Napenda sana na mno Uchapakazi wake Waziri Mkuu wa sasa ( Awamu hii ya Tano ) Mheshimiwa Kassim Majaliwa Kassim ila kuna mahala kama vile naona hapako sawa hasa upande wa mlundiko wa Ratiba zake nyingi ambazo zinahusisha Kusafiri kwa Gari au Ndege ndani na nje ya nchi pasipo hata Kupumzika.
Je, Kiafya hizi Ratiba zake kuwa nyingi nyingi huku zingine zikiwa ni za ghafla haziwezi kuwa na Athari yoyote ile Kwake? Je, kuna ubaya wowote kama kukiwa na Uwiano sawia wa Ratiba za Kikazi na Mizunguko kati yake Waziri Mkuu Majaliwa na Mabosi zake Wawili Wakuu Mheshimiwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Mwamba mwenyewe Rais Dkt. Magufuli?
Kuna muda huwa nahisi kuwa huenda Waziri Mkuu huwa analazimishwa kuwa busy Kiratiba na ndiyo maana wala haihitaji uwezo mkubwa wa Kumsoma na Kumjua kuwa mara nyingi tu hata body language yake huonyesha ni Mtu aliyechoka, aliyeelemewa na Ratiba za Kikazi na Mizunguko ila anashidwa tu Kumwambia Boss wake Mkuu Mheshimiwa Rais labda kwa Hofu ya Kung'olewa.
Yaani asubuhi utasikia yupo Ruangwa, mchana yupo Kisiwandui, alasiri yupo mpakani Namanga na Jioni yupo Ikulu ya huko Bunjumbura Burundi.