Je, hizi chaguzi za ndani CCM zimetuletea faida au zina athari kwa mwenendo wa chama?

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,750
4,958
JE, HIZI CHAGUZI ZA NDANI CCM ZIMETULETEA FAIDA AU ZINZ ATHARI KWA MWENENDO WA CHAMA?

NITOE PONGEZI NA SHUKRANI ZANGU KWA UCHAGUZI WA HAKI, WENYE UTULIVU NA WA BUSARA ULIOTEKELEZWA NA CHAMA CHETU

USHAURI WANGU:
CHAGUZI WA NDANI: Uchaguzi umekwenda vizuri na wanachama wamefanya Maamuzi yao. Ushauri kwa chama changu, wasije wakajaribu kubadilsha matakwa ya wanachama, ili kujiridhisha kwa viongozi wa juu. Mkifanya tofauti na uamuzi wa wanachama basi tunaweza kutana na yafuatayo:

Wanachama wa majimbo wakiona mgombea waliomchagua amefutwa na Viongozi wa juu wa chama, na kumteua kipenzi chao au mtu wa maslahi yao, hapo patakuwa na hatari ya hao wanchama kukasirika na kuja na maamuzi magumu. Kwa kutojitokeza na kumpigia kura mgombea wa upinzani, kwenye uchaguzi mkuu. Tunaweza jikuta wanaCCM wamemchagua mgombea wa ACT au CHADEMA.

Jambo la kufurahiya ni kuwa Watanzania wameamka toka usingizini, Iwapo wameweza kutowapa Kura watu kama Makonda na Gwajima.

Tunajua kazi nzuri na msimamo wa hii awamu ya 5, imekuwa na juhudi nyingi za kuwaelimisha na kuhakikisha wananchi wameamka na wanajua kudai haki zao. Hii juhudi nzuri ya awamu hii, isije ikageuzwa na kutudhuru sie wenyewe, kwa hili nashauri tujichunge na maamuzi yanayoweza kukataliwa na wananchi na kutuaibisha au kutukosesha kura.

Kuna campaign za chini chini zinafanywa na wana CCM, Iwapo , Washindi watatenguliwa, na badala yao wakachaguliwa, wanasiasa vipenzi wa Viongozi au wale waliokuja na SLOGAN ya kuunga juhudi, na kuahidiwa ubunge, basi kuna makundi yanawashauri wapiga kura kutojitokeza kwa wingi, au kutoa kura zao kwa watu wengineo.

Mwenyekiti, muarubaini Mkubwa tuonaowa uchaguzi huu ni timu yetu ya uchaguzi ndani ya chama, kuna watu wanaoamini kutumia Mabavu tena bia haya wala aibu, kuhakikisha ushindi, hawa watu hawajui strategy yoyote, wao ni kutumia mabavu na pesa, na katika pesa kuna Rushwa ya hali ya juu, wanapotumia 1000, unaletewa bili ya 100,000. Tatizo kubwa linaliweza kujitokeza ni watumiapo mabavu, wapinzani na majasusi ya mabeberu, watapata mwanya mzuri, kuuambia ulimwengu kuwa uchaguzi haukua huru. Na hii itakuharibia legacy yako Mwenyekiti na Heshima ya chama chetu.

Wananchi wengi wangependezwa ufanye marekebisho kwenye Timu ya Uchaguzi, iwapo ungewachanganya hawa vijana wa sasa na wazee wenye busara, wavumilivu na wasiokurupuka, ambao hufanya Strategical Planning.

Iwapo ni kweli Lissu ambaye ni tegemeo kubwa la Chadema, Serekali ijitahidi sana kuepuka kumjenga huyu Bwana kisiasa, Polisi wakianza kumuandama, basi kwa UJUMLA wataitumia hiyo rabsha kama kete ya kusema wanaonewa, uchaguzi hauko huru. Tuiwachie Mahakama ifanye kazi zake kwa uweledi.

Wakati kama huu, focus kubwa iko kwenye nchi yetu na sababu kubwa ni uchaguzi, Mahasimu wetu wote na wapambe wao, wamejianda vizuri sana, kurusha video za matendo yoyote yenye vurugu hata kama waanzishi wa hizo vurugu ni wao, na kuziweka kwenye mtandao wa youtube. Mheshimiwa Upinzani wamejitayarisha vizuri sana, na wanauwezo kuyafanya mengi ya kutukashifu bila yasi kujua nani anayehusika. Tusishau vyombo vyetu vya usalama vimechukua muda mrefu sana kuweza kuwanyamazisha, wananchi wetu ambao ni wahasimu wa nchi yao, ambao walikuwa wakitumia mitandao kuijengea nchi yao kashfa na nyingi zilikuwa za kutengeneza.

Tanzania ya uchumi wa kati, hauta imarika vizuri iwapo, hatutazitumia akili nzuri za watanzania wote, na Kama chama kikubwa, kikongwe na Chama cha wengi nchini, hakitajitayarisha vizuri na kuwa na viongozi wa ngazi zote waliokuwa visionaries. Mheshimiwa Rais, huhitaji ngonjera zao za kukusifu, ili hali wananchi wote wanajua juhudi zako na nia yako nzuri kwa nchi yako na wananchi.

Mheshimiwa Kiongozi nayependelea kusemasema Serekali ya Rais JPM iko hivi au inataka hivi au inafanya na kuleta hiki, ni wapambe wasio na self-confidence, na maana inakubidi uwatumbue wengi. “ONE CANNOT PERFORM IF HE HAS ALWAYS TO USE THE POWER THAT IS IN CHAMWINO” Umewa EMPOWER na bado hawawezi timiza wajibu wao mpaka watumie jina la Rais, sasa uwezo wao utakuwa wapi.

Mheshimiwa tunataka Serikali yako ijayo iwe na Vijana real performers na sio wasifiaji tuu. Hawa wa sasa wanaamini wakikusifu sana, basi ndio kinga ya kutotumbuliwa.
 
Ccm wamwshindww kukusikiliza ushauri wako na kumleta tapeli Gwajima.

Sasa tunasema hivi, tunakwenda kumalizana na ccm tarehe 28.
 
Zimesababisha Chama chetu cha CCM kufariki na maziko yake rasmi tarehe 28/10/2020 ,ni msiba mkubwa. Wenye meza na viti wote presha zao zipo juu sana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom