Je, hili Tangazo la Tigo linalotuhimiza kupata cha 'Asubuhi cha Tigo' TCRA na Serikali wamelibariki na kuona limekaa Kimaadili?

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,375
2,000
kiuhalisia TCRA inatakiwa ikiona maneno yanayotumika kwenye matangazo kama hayo ambayo yanaendana hata kwa misemo ya kiswahili potofu wayazuie kuleta heshima siyo vizuri maneno kama hayo kuyabariki hivi unajisikiaje asubuhi mnajiandaa kwenda kazini upo na watoto wako sebueni linakuja tangazo kama hilo kweliiii watoto wanapata picha gani kwamba mzee anahimizwa akamkandamize mother cha asubuhi? noma sana

Hili lipo mpaka ktk vyombo vya habari magazeti, vituo vya tv, stesheni za radio n.k

Inaonesha watangazaji, waandishi wa habari, wataalamu wa habari na mawasiliano, wasanii, wanamuziki, sisi watumiaji wa mitandao ya kijamii pamoja na watengeneza matangazo tunakabiliwa na upungufu ktk umahiri wa kutumia lugha na kutafuta njia ya mkato kuwasilisha ujumbe.
 

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
1,376
2,000
Hizi akili hizi,niambie kwenye maneno "Cha asubuhi"tusi lipo wapi?
Tusi limejaa kwenye kichwa chako,maana unawaza ngono tu,inawezakana ni Cha asubuhi kifurushi,Cha asubuhi kikombe Cha chai!
Hii ni Sawa waliopiga kelele wimbo wa Nyegezi upigwe marufuku,lakini walivyo wajinga,Kuna sehemu nchi hii inaitwa Nyengezi stand,nyegezi Kona.
Kama unasema "Cha asubuhi"ni matusi,vipi kuhusu "makunduchi"mchamba wima"
Na haya ni majina ya vitongoji kule Zenj!
Acha ujinga.
Mpemba anaitamka hivi"makunduuchi;.
 

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,782
2,000
Hilo tangazo naona watu wazima ndio wanawafundisha watoto wajiulize hiki cha asubuhi ni kitu gani, na wakikipata msije tena kulalamikia mimba za utotoni.

Kama shida ni "cha asubuhi" hata kikombe cha chai ni cha asubuhi pia, japo kinaweza kutumika na jioni pia.
Ila si tayari wameruhusu wanafunzi kuendelea na masomo hata wakipata ujauzito??
 

chivala

JF-Expert Member
Apr 13, 2021
751
1,000
Nimekaa zangu nawaza niende kwaya,mara nikasikia tangazo la tigo wanahamasisha Cha asubuhi.kusema kweli nimewaza mbali akili yangu ikawazaaa.sijui Kama nitalala home leo niombeeni tu.namba nilishablock ila namtafuta kwenye file la emergency
Tigo mlaaniwe
Kwani kwenye tangazo lao, wanamalizia na piga show ya asubuhi? na hata kama si jiwe moja kuuwa ndege wawili!
 

Holy Man

JF-Expert Member
Feb 4, 2021
4,315
2,000
Nimekaa zangu nawaza niende kwaya,mara nikasikia tangazo la tigo wanahamasisha Cha asubuhi.kusema kweli nimewaza mbali akili yangu ikawazaaa.sijui Kama nitalala home leo niombeeni tu.namba nilishablock ila namtafuta kwenye file la emergency
Tigo mlaaniwe
Hapa nipo njiana naelekea Juliana 🤭🤭
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom