Je, hili Tangazo la Tigo linalotuhimiza kupata cha 'Asubuhi cha Tigo' TCRA na Serikali wamelibariki na kuona limekaa Kimaadili?

Hata mawazo mgando, cha asubuhi ubaya upo wapi? acha kuwaza ngono waza pesa utakufa masikini wewe.
kwanza tujiulize, umaarufu wa hili neno 'cha asubuhi' umetokana na nini? kama umetokana na mitazamo ya kingono ina maana tiGo wamecopy huo msemo kutokana na umaarufu wake!

Tukikaa kimya, kesho na keshokutwa, Voda nao watakuja na slogan ya 'mpelekee moto' nao watasema kwani kuna ubaya gani...... tutaendelea kuwa jamii ya kipuuzi.
 
Hili tangazo la TIGO ... CHA ASUBUHI... linadhihirisha mmomonyoko wa maadili. Serikali ya mama SSH ilione na kulikemea haraka sana. Tusirasimishe lugha za matusi. Kama serikali ilipiga marufuku matangazo ya FATAKI, wimbo Magendaheka kwanini tuendelee kusikia hili tangazo la hovyo...

Say No #ChaAsubuhi.
Samahani kwani CHA ASUBUHI lina maana gani katika muktadha wa lugha bila kuweka dhana ya kipotoshaji kumaanisha "kufanya mapenzi asubuhi"

likisimamama neno lenyewe lina UKAKASI gani??
 
Jamani mtoa Uzi hata hajataja neno ...ngono ..katoa ushauri wa Tangazo la Tigo lipigwe marufuku...ajabu wachangiaji wengi tunataja neno...NGONO...!!!!
 
Hili tangazo la Tigo 'Cha Asubuhi' linadhihirisha mmomonyoko wa maadili. Serikali ya Rais Samia ilione na kulikemea haraka sana. Tusirasimishe lugha za matusi. Kama serikali ilipiga marufuku matangazo ya Fataki, wimbo Magendaheka kwanini tuendelee kusikia hili tangazo la hovyo?

Say No #ChaAsubuhi.
Hizi akili hizi,niambie kwenye maneno "Cha asubuhi"tusi lipo wapi?
Tusi limejaa kwenye kichwa chako,maana unawaza ngono tu,inawezakana ni Cha asubuhi kifurushi,Cha asubuhi kikombe Cha chai!
Hii ni Sawa waliopiga kelele wimbo wa Nyegezi upigwe marufuku,lakini walivyo wajinga,Kuna sehemu nchi hii inaitwa Nyengezi stand,nyegezi Kona.
Kama unasema "Cha asubuhi"ni matusi,vipi kuhusu "makunduchi"mchamba wima"
Na haya ni majina ya vitongoji kule Zenj!
Acha ujinga.
 
Unaowaambia wapige marufuku ndiyo wenye hisa humo, kumbuka "jaza ujazwe"
 
Hizi akili hizi,niambie kwenye maneno "Cha asubuhi"tusi lipo wapi?
Tusi limejaa kwenye kichwa chako,maana unawaza ngono tu,inawezakana ni Cha asubuhi kifurushi,Cha asubuhi kikombe Cha chai!
Hii ni Sawa waliopiga kelele wimbo wa Nyegezi upigwe marufuku,lakini walivyo wajinga,Kuna sehemu nchi hii inaitwa Nyengezi stand,nyegezi Kona.
Kama unasema "Cha asubuhi"ni matusi,vipi kuhusu "makunduchi"mchamba wima"
Na haya ni majina ya vitongoji kule Zenj!
Acha ujinga.
Sijui unajua nini ila niruhusu nikuarifu kuwa maana hutengenezwa na mpokea ujumbe. Kama mpokea ujumbe kasema ujumbe wako una ukakasi huna namna. Wacha Tigo wazibe masikio ila madhara yake siyo ya leo wala kesho ytakuwa ni madhara ya kudumu
 
kwanza tujiulize, umaarufu wa hili neno 'cha asubuhi' umetokana na nini? kama umetokana na mitazamo ya kingono ina maana tiGo wamecopy huo msemo kutokana na umaarufu wake!

Tukikaa kimya, kesho na keshokutwa, Voda nao watakuja na slogan ya 'mpelekee moto' nao watasema kwani kuna ubaya gani...... tutaendelea kuwa jamii ya kipuuzi.
Hakuna tatizo kwenye tangazo bali tatizo ni watafsiri wa Tangazo na katika hili nawapongeza tigo kwa kuwa wabunifu... hata mtando wao kuuita tigo kuna watu wanaona ni shida na ni tusi kwa sababu wanawaza ngono.
Tigo wamefanikiwa na nina wapongeza sana kwenye hili
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom