Je,Hili limekaaje kidiplomasia?

Tony antony

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
4,988
3,268
Habari wanajf....

Leo wakati nasikiliza hotuba ya Mhe.Rais JPM nilipata kumsikia akisema bado, atasimamia msimamo wake wakufuata sheria kwa mifugo yote itakayoingia nchini kutoka nchi jirani, hii ikiwepo na pamoja na kile alichokitekeleza mhe.waziri kwa kupiga mnada ng'ombe kutoka Kenya kwa ruhusa ya mahakama ya Tz, pamoja na kukamata wale ng'ombe 6000+ kutoka Uganda.

Mbali na hiyo akaongeza kuwa hata mifugo yetu kutoka nchini ikiingia nchi jirani nayo nchi hiyo ifuate taratibu zao za kuwadhibiti hiyo mifugo kulingana na sheria zao.

Swali langu,je hii kidiplomasia imekaaje na ukizingatia ujirani wetu na desturi zetu za kuvuka mipaka kipindi cha kiangazi kulisha mifugo nchi jirani na kurudi??

Na je haya mambo yataishia kwenye mifugo tuu hayataenda mbele zaidi ya hapa??
 
Back
Top Bottom