Je hii ni serikali ya CCM? AU ya Jamhuri ya Muungano

wishega

Member
Sep 6, 2010
7
0
JE HII NI SERIKALI YA CCM?
Ndugu zangu kuna jambo naona tukiliacha liendelee hivi linavyoendelea linaweza kutuletea shida baadae,nalo ni hili la wabunge wa CCM na msemo wao wa Serikali ya CCM.Wamekuwa wakisema hivi mara kadhaa hasa wanapokuwa wakichangia hoja mbalimbali bungeni.

Hili si jambo geni masikioni mwa watanzania hata katika mkutano wa bunge unaondelea mjini Dodoma,mara kadhaa tumewasikia wabunge kadhaa kupita CCM wakiisifu Serikali kwa kusema Serikali makini ya CCM,Serikali sikivu ya CCM,Serikali hodari ya CCM nk.

Hoja yangu hapa si kupinga au kubeza kuwa Serikali haijafanya jambo lolote zuri kwa kipindi cha takribani miaka 50 tangu tupate Uhuru, lah hasha. Serikali imefanya mazuri mengi tu yakiwemo kuongeza idadi ya vyuo vikuu vya umma,shule za sekondari na msingi,zahanati na vituo vya afya,barabara za kiwango cha lami nk.Ila hoja yangu hapa ni kwmba Serikali hii si CCM bali ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2005,Ibara ya 34(1) Kutakuwa na Serikaili ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yetu ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano,na pia mambo mengine yote yahusuyo Tanzanaia bara. Ibara hii haisemi kuwa kutakuwa na Serikali ya CCM au chama chochote cha siasa.

Hivyo ni vema wabunge wanaotokana na CCM wakaelewa kuwa Serikaili hii ni ya Jamhuri w Muungano na CCM chama kilichopewa dhamana ya kuiongoza tu na wala si Serikali yao.Kwani usemi huu unaondelea hivi sasa hauwatendei haki wananchi wengine wasiowanachama wa chama chochote cha siasa. Kwani si watanzania wote ni wanachama wa vyama vya siasa,wengine si wanachama aidha kwa hiari yao au kwa masharti ya kazi zao.

Tukiendelea na usemi huu wa kusema ni Serikali ni ya CCM tunaweza wavunja moyo watumishi wengine ambao si wanachama wa CCM ambao kimsingi hao ndio watekelezaji wa Ilani ya chama cha tawala,Je kwa kudhani kuwa kumbe Serikali hii ni wana-CCM hakutowavunja moyo?. Katiba yetu ya Tanzania ibara ya 35(1) Shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba ya Rais. Je usemi
Huu wa Serikali ya CCM utakuwa na matokeo gani kwa watumishi ambao si wafuasi wa vyama vya siasa?

Waheshimiwa wabunge wanatokana na CCM na wanachama wa CCM ,hebu muanze sasa kubadili fikra na mawazo yenu ya kudhani kuwa Serikali hii ni ya CCM,Serikali hii ni Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania hivyo ni yetu sote na mali ya chama fulani cha siasa vinginevyo. Jambo la msingi hapa ni kuwa CCM imepewa dhamana na watanzania walio wengi kupitia Uchauguzi wa mwaka Oktoba, 2010 kuingoza Seriakali hii ni wala si Seriakali yao na kamwe haitokuwa Serikali yao.

Nihitimishe kwa kusema kuwa tuache kauli zinazoweza kutugawa kwani Tanzania hii ni yetu sote tuungane kwa pamoja kufanya kazi kwa ustawi wa Taifa letu bila kujali tunatokea chama gani cha siasa,dini gani,dhehebu gani,kabila gani na vitu kama hivyo.

Na, Mboyi Daniel Wishega
0712-840525 na 0759-313908
Email;mboyi_wishega@yahoo.com
 
Kama usingekuwa mgeni wa siasa usingeshangazwa na hilo. Ukienda Uingereza utaambiwa the labour au conservative government na Marekani utaambiwa the democratic or the Obama administration. Ni namna ya kutambulisha chama kilichounda serikali ambayo kwa wakati huo iko madarakani. Kama wewe unakereka na matamshi hayo hata kupata shida ya kuchambua katiba, basi uje unapata shida isiyo na sababu maana hata wakati wa kampeni Slaa alikuwa akisema "serikali ya Chadema itaondoa ushuru au kodi ya vifaa vya ujenzi n.k", na wala haikuwa dhambi. Panua mtazamo na punguza munkari wa kichama.
 
JE HII NI SERIKALI YA CCM?
Ndugu zangu kuna jambo naona tukiliacha liendelee hivi linavyoendelea linaweza kutuletea shida baadae,nalo ni hili la wabunge wa CCM na msemo wao wa Serikali ya CCM.Wamekuwa wakisema hivi mara kadhaa hasa wanapokuwa wakichangia hoja mbalimbali bungeni.

Hili si jambo geni masikioni mwa watanzania hata katika mkutano wa bunge unaondelea mjini Dodoma,mara kadhaa tumewasikia wabunge kadhaa kupita CCM wakiisifu Serikali kwa kusema Serikali makini ya CCM,Serikali sikivu ya CCM,Serikali hodari ya CCM nk.

Hoja yangu hapa si kupinga au kubeza kuwa Serikali haijafanya jambo lolote zuri kwa kipindi cha takribani miaka 50 tangu tupate Uhuru, lah hasha. Serikali imefanya mazuri mengi tu yakiwemo kuongeza idadi ya vyuo vikuu vya umma,shule za sekondari na msingi,zahanati na vituo vya afya,barabara za kiwango cha lami nk.Ila hoja yangu hapa ni kwmba Serikali hii si CCM bali ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2005,Ibara ya 34(1) Kutakuwa na Serikaili ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yetu ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano,na pia mambo mengine yote yahusuyo Tanzanaia bara. Ibara hii haisemi kuwa kutakuwa na Serikali ya CCM au chama chochote cha siasa.

Hivyo ni vema wabunge wanaotokana na CCM wakaelewa kuwa Serikaili hii ni ya Jamhuri w Muungano na CCM chama kilichopewa dhamana ya kuiongoza tu na wala si Serikali yao.Kwani usemi huu unaondelea hivi sasa hauwatendei haki wananchi wengine wasiowanachama wa chama chochote cha siasa. Kwani si watanzania wote ni wanachama wa vyama vya siasa,wengine si wanachama aidha kwa hiari yao au kwa masharti ya kazi zao.

Tukiendelea na usemi huu wa kusema ni Serikali ni ya CCM tunaweza wavunja moyo watumishi wengine ambao si wanachama wa CCM ambao kimsingi hao ndio watekelezaji wa Ilani ya chama cha tawala,Je kwa kudhani kuwa kumbe Serikali hii ni wana-CCM hakutowavunja moyo?. Katiba yetu ya Tanzania ibara ya 35(1) Shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba ya Rais. Je usemi
Huu wa Serikali ya CCM utakuwa na matokeo gani kwa watumishi ambao si wafuasi wa vyama vya siasa?

Waheshimiwa wabunge wanatokana na CCM na wanachama wa CCM ,hebu muanze sasa kubadili fikra na mawazo yenu ya kudhani kuwa Serikali hii ni ya CCM,Serikali hii ni Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania hivyo ni yetu sote na mali ya chama fulani cha siasa vinginevyo. Jambo la msingi hapa ni kuwa CCM imepewa dhamana na watanzania walio wengi kupitia Uchauguzi wa mwaka Oktoba, 2010 kuingoza Seriakali hii ni wala si Seriakali yao na kamwe haitokuwa Serikali yao.

Nihitimishe kwa kusema kuwa tuache kauli zinazoweza kutugawa kwani Tanzania hii ni yetu sote tuungane kwa pamoja kufanya kazi kwa ustawi wa Taifa letu bila kujali tunatokea chama gani cha siasa,dini gani,dhehebu gani,kabila gani na vitu kama hivyo.

Na, Mboyi Daniel Wishega
0712-840525 na 0759-313908
Email;mboyi_wishega@yahoo.com

Sio kosa lako, unaonekana kuwa ni mwana sayansi na si mwanasiasa au umesoma sana Chemistry. hii ni serikali ya Muungano inayoongozwa na CCM. hivyo kusema serikali ya CCM ki siasa ni sahihi tu.najua unatamani sana kusikia neno "serikali ya Chadema" ni ndoto.
 
Back
Top Bottom