Je hii ni sawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je hii ni sawa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by 4X4byfar, Nov 3, 2008.

 1. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2008
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wapendwa mimi ndio mara yangu ya kwanza kuwa hapa. Nina jambo naombeni msaada.

  Nimeolewa hivi karibuni, baada ya kumjoin my husband aliamua kuni tambulisha kwa wanawake aliye dai ambao baadhi ni marafiki tuu wakawaida na wengine ni wafanyakazi wenzake. Ok nilikubali na kuwaona wote. Ila sasa nimekaa mda wengine wakawa wanampigia simu mara kwa mara wakiwa anaongea nao (kukopa kadi ya basi,majani ya chai, kubadilishana mboga, Kuwapa more concentration when out in a party, kuwapa lifti mpaka nyumbani kwao...) kweli hili jambo likawa likinikera sana, ikafika siku tuligombana sana na kumwambia achane na hayo mawasiliano na hao wanawake au niachane naye. Sasa yeye badala ya kukubali alibakia kubisha sana na kuniambia hana uhusiano nao wowote. Je nilifanya kosa kumwambia hivyo, na je mtu anapooa si ndo kuachana na ukapera jamani?
   
 2. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2008
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mhhh sound kama hamjuani hivi lakini,anyway sasa dada hapo hata mimi nitashiondwa kukuelewa kidogo maana inaonyesha hamjuani au sio...Inavyoonekana katika habari yako hapo juu kwamba mmekutana na kuowana si ndio???Ok kama unamjua na unasema mmeowa je toka hapo zamani ulikuwa hujui kama husband wako ana wanawake wengine ambao alikuwa anafahamiana nao??Ok lakini umefanya vizuri kumueleza ukweli kwasababu wewe ni mke so sio mbaya sana ila kama umemuambia aache itachukuwa time kwake kuacha hivyo vitu maana nadhani umevikuta so haitakuwa rahisi kuacha papo hapo ila cha zaidi ni kuvumilia tu basi...
   
 3. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ni vema ukamuelewa mumeo vizuri. Pia inaonekana kama hawa mabinti wapo wengi kama 10 vile au zaidi, jifunze nyendo za mumeo zidi yao labda "anakula na kipofu na sasa anataka kula tonge la mwisho". Wakati mwingine anaweza kuwa sio hivyo, lakini la muhimu jifunze nyendo, tabia na muelewe mumeo.
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  One more reason not to get married fellas, that is, if you are trully not ready for commitment.

  Jamaa anawakia pembeni, mamaa ana machale na rightly so, sasa kama alitaka uhuru wa kutomasa pembeni alioa kwa sababu gani?

  Ndoa ni sakramenti takatifu, na kama mke wa kaisari ilikuwa hatakiwi hata kushukiwa kwamba ana uhusiano nje ya ndoa, kwa nini mume wa huyu dada atake kuwa na uhuru utakaomletea mkewe wasiwasi? regardless ya ukweli kwamba hawa wanawake ni marafiki tu au kuna jambo zaidi, kama mke wako hafurahii unaacha, ndiyo mana ya ndoa.Ama sivyo kama alitaka kuendelea na uhuru wake alioa kwa nini?

  One more reason not to get married fellas, I know I ain't.

  Ukitaka kumla nguruwe chagua aliyenona, ukitaka uhuru chagua ukapera, siyo unajifunga kwa ndoa halafu unataka vya nje tena...
   
 5. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2008
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli kujuana kwetu ni kwa dot com, nadhani umenipata so nilipo kuja huku anapoishi ndo nikakumbana na hayo mambo.
   
 6. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2008
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hao wanawake ni zaidi ya hao 10, kwa kweli nyendo zake ndizo zilizoanza kunitia wasiwasi. Maana anaweza kusema anaenda kwenye kikao then akarudi saa nane usiku na stori kibao.
   
 7. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2008
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Ok sawa sawa hapo sasa nimekuelewa vizuri maana kwanza nilikuwa nataka kushangaa inakuwaje hapo.....Ok ungesema toka mwanzo ningekuelewa vizuri.Hapo cha muhimu ni kumuweka chini mume wako na kumuambia ukweli live basi wala usilembe maana ukikaa kimya unacheka cheka utashangaa analala nje ukimuuliza ulikuwa wapi atakuambia kwa marafiki zangu so dada kuwa na msimamo na penzi langu na kuwa muwazi kwa mume wako wala usimuogope kumwambia kitu atajirekebisha tu......
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Mume wako ni Mtanzania? Mwambie hupendi uhusiano na hao wanawake wanaompigia simu kila wakati na yeye kuwabeba na gari lake kila mara. Ni lazima akuheshimu kama hawezi kufanya hivyo basi hii ndoa haitakuwa na maisha marefu. Na hivi vikao anavyoenda ni vikao vya nini hasa. Mwanaume kwenda kutembea na usiku ni jambo la kawaida lakini vikao kila mara tena anakutana na hao wanawake kwenye hivyo vikao. Una haki machale yanavyokucheza.
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Hii ngumu sana. Lakini kama amekutambulisha sidhani kama kuna kitu hapo, sijui lakini sijawahi kuoa. Eti unaweza ukamtambulisha nanihino kwa wife jamani?

  Sasa hizo party na wewe si uunge msafara mama!
   
 10. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mamaa,pole sana,nafikiri utakuwa nchi za watu ,pole sana,inawezekana kabisa alivyokuwa single alikuwa ni mkarimu sana na alikuwa lonely pia,so wanawake waliweza kumzoea ,na itakuwa kazi sana kuachana nao maana mumeo anaoeneka yuko weak kenye hilo swala,endelea kukaza uzi huohuo mama,pia kuwa naye karibu kila wakati,hata hao wanawake watasogea pembeni maana atakuwa busy na wewe zaidi,endelea kumwelesha maadili mema pia,si unajua tena alishajisahau ,na kama ndio mpole basi tena wanawake walishamteka.
   
 11. h

  hekima New Member

  #11
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  karibu sana dada yetu na pole kwa tabia za "kutowajibika" za mume wako. kwa kifupi na kwamba,swali kama hili linahitaji jibu la makini na la ukaribu.nadhani site hii si wala si rahisi kupata ushauri utakao kufaa kwa swala la kijamii,kifamilia na kimahusiano kama hilo.yawezekana wengi kati ya watakao kujibu wana tabia kama hizo, hawatokupa ushauri utao kufaa. uliza swali hili kwenye website za kijamii na kidini utapata msaada wa kutosha.
   
 12. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2008
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana ndugu kwa maoni na ushauri wako mzuri, nikweli kabisa uliyoyasema humu katika hiki kipengele. Sasa nilikuwa naomba kama hizo website unaweza kunitumia ili nifatilie zaidi ntashukuru sana. Ubarikiwe kwa moyo wako mzuri.
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hekima,
  Your wrong!
  Hapa unadhani wako watu wasio na status ya kumjibu the right answer?
  Si kweli kila aliye hapa anapitia njia hizo. Hapa kuna kila vipaji kwa taarifa yako. Cha muhimu nikuangalia nini anashauriwa na afuate ushauri mzuri tu. Huko unakomuagiza nakwambia pia ni shida tupu maana wengine huko ni washauri lakini pia ni yaleyale tu.
  Ni kweli yawezekana wengine wamepitia njia hizo na wanaweza ku provide jibu sahihi kabisa.
  Sikiliza 4x4byfar hiyo ndiyo ndoa na ugumu wake na hasa unapofika mahali pa kuolewa na mtu kwa kutomfahamu vizuri. Wonderfully watu huwa wanabadirika. Mvumilie sana mmeo na katika kipindi hiki ongeza pendo na sio chuki wala uhasama huku ukijifanya ujali.
  Lakini pia katikakipindi hicho kitumie kumuelekeza katika upendo nini ufurahii na nini unafurahia.
  Nimeona baadhi ya wakina mama wanatumia hata hiyo 6X6 kumalizia hasira zao. Utumia kila ufundi wa kimapenzi kumuweka mmewe sawa. Hapo nadhani unanipata.
  Kila mwanaume kwa taarifa huwa ana mademu nje lakini?????? ukishaoa tu mahusiano yoooooote yanaisha siku ya wedding. Unawatangazia wote kuwa kuanzia leo baaaaaaaaaaaaasi.
  Wengine nimeona wakiacha tabia hii taratibu.
  I am sorry to admit this, kwamba mimi pia nilikuwa na tabia kama ya mmeo hadi nilipompokea Yesu kama mwokozi. Nikatubu na kuacha.:D
   
 14. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ushauri

  Bado naamini kabisa ,anaweza kurekekebishika,wewe mweleshe HE IS NOT RIGHT...
  Yeye alikuwa ameshazoea maisha hayo,na bado nasisitiza huyo atakuwa hayuko strong,sasa mamaa kuanzia now ,kuwa strict ,hapo hamna mchezo ,kwambinu zozote,si unampenda mumeo bwana,anza leo,kwambinu zozote ,naamini ua mature enough kwa kumwelewesha hiyo sio njia sahihi,taratibu atajirudi tu,

  na hawao wakina dada waweke sawa(msinione rude),dunia ndivyo inatakiwa iwe sasa hivi,mimi nilikuwa mtu wa kukaa kimya nimeathirika kisaikolojia sana,so MaMaa Stop them now!!!!!hakuna cha upole wala nini,shida zote ni wewe unazibeba sasa hivi ,unless kama wanakusaidia hawo wanawake-THE BIG NO!!!!!!!!
   
 15. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2008
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  unajua watu saa zingine huwa wanasahau shilingi ina pande mbili mpaka wakumbushwe...
  tell him to put himself in your shoes halafu aone anajisikiaje...yaani ungekuwa ndio wewe umemtambulisha kwa rafiki zako wa kawaida na wafanyakazi wenzio wakiume , halafu wakaanza kukupigia simu mara kwa mara.. 'kukopa kadi ya basi,majani ya chai, Kuwapa more concentration when out in a party, kuwapa lifti mpaka nyumbani kwao' angejisikiaje? mwambie jinsi anavyojisikia vibaya hata kuimagine kitu kama hicho na wewe pia unajisikia vibaya
   
 16. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2008
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  My dear contributor asante sana kwa ushauri wako mzuri sana. Kuna siku nilimwambia hivyo hivyo ( what if yeye ndo angelikuwa namfanyia hayo yote would happen) Jibu nililopewa ni kwamba mimi nimeshajenga hayo hisia na mawazo so nilizima nifikirie hivyo. Natoka nimwambie huo ukweli kwa kweli amebadilika sana huwezi amini tunaweza kutoka kwenda nje (church, shopping...) nakwambia anauchuna, hacheki na mimi. Nikianzisha topic anajibu kimkatokato tuu mara nikitaka nielekezwe kitu ni kama hataki. Kwa kweli inaniuma sana. Pengine na mimi nikisema niuchune ndo kwanza kama haelewi kabisa. Jamani nishaurini kwenye hili maana nimejikuta na mimi naishiwa na hisia na yeye.
   
 17. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #17
  Nov 8, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mumeo Mtanzania?
   
 18. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #18
  Nov 9, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Toa usaidizi, akiwa mhindi au mzungu unampa ushauri gani! haya sema sasa.
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  Rukia 6*6 by far utaona atakavyohangaika...
  Mpige sala za mara kwa mara na kila akiondoka akrudi muombe roho mtakatifu akuonyeshe njia akirudi anakuta unanena luha ya mbinguni shakarabo shundarabo ukimlilia mungu bila kuchoka huku unamfungulia mlango na kumwamabia mungu kama ni wangu mbadilishe kama si mapenzi yako
  muondoe kabisa!!!jamani biblia inasema adui yako muombee afe ila huyu muombee aondoke ,mungu akutafutie wako dada,ngoja nikupe kisa kimoja cha maisha yangu'

  nilioa mwaka 2005,,mwezi wa kuminamoja pale azani nikafanya sheehe pale diamond jubilee ,aliekuwepo alijua tunacosubiri ni pepo tu,,nilipokaa ndani na mkewangu aikuchukua muda ,nikawa mtu wa mamombi sana ,,la hasha mwezi wa pili mungu akanza kunionyesha jinsi yule mwanamke alivyoa,,aje amelewa na akuwahi kunywa miaka 2,mara sigaraaje na rafikizake aliokuwa anasoma nao nje wanavuta sigara nyumbani,,,nilimweleza ukweli nikajua hapa napambana na nguvu za giza,,nikasalisali sana mwisho uovu ukazidi kuelekea ukahaba!!!ndipo nikaamua kuamia chumba kingine na kumwambia mungu nipe nafasi niweze kuondoka kwa amani!!!kama ni mke wangu ulienipangia ntakaa nae else niweke pembeni nae kabisa kabisa,,mwaname akazidisha akaenda nje bila kumwaga aliporudi nikwamwaga kwa amani ,,nikamwambia mungu msaidie apate uliempangia na mi nipe atakaenifaa
  nimeishi muda wote huo ndugu mwaka huu nikakutana na dada mmoja ,niko nae urafik namwomba mungu afunue milango ,usikate tamaa mwombee mema hata mkiachana,,jamani ukiwa na mungu akuna kinachoshindikana ,unakuwa na mamlaka makubwa ya kuamuu hata adui yako afanywe nini!!!!

  Piga goti mama kumekucha!!!!!ntajaribu kuja kukupa maneni ya mungu yatakayokusaidia mara kwa mara kumuaibisha huyo shetani wa anaemsubua huyo mumeo!!!!

  Mafanikio mema!!!
   
 20. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2008
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nashukuru ndugu kwa mchango wako mzuri na wa kutia moyo kwa kweli. Hapo juu nimebold red kipengele fulani kimenigusa kweli. Naomba unipemaandiko yanapatikana wapi ili nisome pia. Ntashukuru kwa maombi yako na msaada wako ndugu. Kwa kweli shetani anatakiwa kuaibishwa. Ubarikiwe.
   
Loading...