Je, hii ni njia sahihi ya kusafisha uume baada ya haja ndogo?

Wakitoka hapo wana shake hands na wewe, baadavya hapo una nunua vitumbua unakula. Ndiyo maana Tanzania tunapendana sana
Ho ho ho! Sina mbavu, hiyo tu. Ikitoka kupapuchua pia haioshwi. Tunashake hands tu!
 
Kabla ya ku shake Tanakamua
Mkojo wote, na Baada ya ku shake inabaki kaz ya chupi kufuta unyevu uliobaki,
So hamna shida coz mikono na chupi vinafanya kaz ya maji na sabuni,
Ndio maana style ya Choo za wanaume Ziko mbili na bafu ni ya tatu ya haja kubwa, haja ndogo, na bafu.
Wamama wanna style moja tu ya Choo na bafu.
Kwahiyo kutonawa unavyotoka haja ndogo ni sawa kwa vile maumbile yanaruhusu
 
  • Thanks
Reactions: o_2
Kwa wanaume wote, imekua kawaida sana baada ya kujisaidia haja ndogo, tunatikisa (shake) uume kama ndio njia ya kujisafisha au kutoa mkojo unaobaki.

Je, hii ndio njia sahihi au?


Hapana sio njia sahihi.
Tunatakiwa kutumia maji.
Kama hakuna bas hata Toilet paper, majani au jiwe.
[HASHTAG]#myopinions[/HASHTAG]
 
Wakitoka hapo wana shake hands na wewe, baadavya hapo una nunua vitumbua unakula. Ndiyo maana Tanzania tunapendana sana
ndo maana siku hizi chakula kinachohitaji mkono natumia left hand sitaki upuuzi mimi wakulishana mikojo na mavi ya watu
 
Kwa sisi waumini wa dini ya Kiislam, unatakiwa mwanaume kukojoa kwa kuchuchumaa, baada ya hapo uoshe hiyo dhakari "dudu" kwa maji safi kuondoa najisi ya mkojo.
Baada ya kumaliza haja zako unawe mikono kwa maji safi
Inapotokea dharula basi unaweza kustanji kwa mawe matatu (naweza sahihishwa) kuondoa mkojo kwani ni najisi. Hii ina maana inaepusha chupi kuwa na mikojo ilhali unatakiwa kufanya ibada
"Uislam ni usafi"! Nawasilisha
Baada ya kutumia hayo mawe unayaweka wap mkuu?
 
Mawe utayaandaa kabla ya kukojoa. Ni lazima uzingatie baadhi ya mambo kabla ya kukojoa na haifai kukojoa hovyo hovyo si kidini tu bali hata kistaarabu. Usikojoe chini ya mti wa kivuli, usikojoe jalalani, usikojoe pembeni ya shimo wala usikojoe sehemu ngumu ambayo itafanya 'cheche za mkojo kukurukia' mwilini mwako
Kwa faida zaidi juu ya kustanji soma hapa chini

KUSTANJI

Inajuzu/inafaa kustanji (kuchamba) kwa kutumia maji mutlaq (maji halisi) ambayo ndiyo asili katika kujitwahirisha na najisi. Pia inajuzu kustanji kwa kila kitu chenye sifa zifuatazo :

i.Kigumu (kigogofu)

ii.Chenye Kuparuza (kisichoteleza)

iii.Kinachoweza kuondosha najisi.

Vitu vyenye sifa hizi ni kama mawe, karatasi, kitambaa na kadhalika.

Ni vema kustanji, mtu akaanza kwa kutumia mawe/karatasi kisha ndio akamalizia na maji.

Kufanya hivyo ni kwa sababu mawe/karatasi huondosha juta (dhati) ya najisi na maji huondosha athari ya najisi bila ya kuchangayika na juta lake.

Ikiwa atatumia kimojawapo baina ya mawe/karatasi na maji, basi ni bora akatumia maji kwani ndiyo pekee yenye uwezo wa kuondosha juta (dhati) na athari ya najisi, kinyume na mawe na nduguze {karatasi, kitambaa na kadhalika}.

Imepokelewa kutoka kwa Anas Ibn Maalik – Allah amuwie Radhi – amesema :

Mtume wa Allah alikuwa akiingia mahala pa kukidhi haja, mimi na kijana wa rika langu tukimbebea chombo cha maji na fimbo/mkuki mfupi, basi akistanji kwa kutumia maji. Bukhariy na Muslim.

Maelezo : Fimbo/Mkuki ulikuwa ukitumika kama sitara na alama wakati wa kuswali ili mtu asiweze kupita mbele.

Imepokewa na Ibn Masoud – Allah amuwie Radhi – amesema :

Mtume – Rehma na Amani zimshukie – alienda kukidhi haja na akaniamrisha nimletee mawe matatu. Al-Bukhariy.

USISTANJI kwa kutumia najisi nyingine iliyo kavu au kitu kilichonajisika tayari kwani huenda kikaizidisha athari ya najisi badala ya kuipunguza.

Kadhalika ni haramu kustanji kwa kilicho chakula cha binadamu kama vile mkate au chakula cha majini kama vile mifupa. Amesema Bwana Mtume – Allah amshushie Rehma na Amani –

"Msistanji kwa (kutumia) kinyesi cha wanyama wala mifupa kwani hiyo (mifupa) ni chakula cha ndugu zenu majini" Tirmidhiy.

Hakika MWENYEZI MUNGU ANAJUA ZAIDI.
hahah aisee mjomba umenifurahisha sana.

Ngoja nianze Kutembea na mawe matatu kwa ajili ya JUTA,hahah
 
Kwani kuna aliye na ushahidi kwamba alishawahi kudhurika kwa kutumia njia hii ya ku shake after use.
 
Wakitoka hapo wana shake hands na wewe, baadavya hapo una nunua vitumbua unakula. Ndiyo maana Tanzania tunapendana sana
Tunatumia kushoto kushake mkojo uliobaki,na tunashake hands for greeting na mkono wa kulia,na tunaponunua vitumbua tunakula kwa kutumia right hand.
 
Back
Top Bottom