Je, hii ni njia sahihi ya kusafisha uume baada ya haja ndogo?

Wakitoka hapo wana shake hands na wewe, baadavya hapo una nunua vitumbua unakula. Ndiyo maana Tanzania tunapendana sana
Na Mimi nilisha shake na wewe kwenye harusi moja hivi, wakati natoka kushake chooni na wewe unaelekea huko, remember me?
 
Wakitoka hapo wana shake hands na wewe, baadavya hapo una nunua vitumbua unakula. Ndiyo maana Tanzania tunapendana sana
Kuna shida gani kama huwa mnanyonya na mnasemaga wenyewe koni sa ushaona mtu anaosha koni ndo ale
 
Kwa wanaume wote, imekua kawaida sana baada ya kujisaidia haja ndogo, tunatikisa (shake) uume kama ndio njia ya kujisafisha au kutoa mkojo unaobaki.

Je, hii ndio njia sahihi au?
Kama wewe ni ME jibu unalo. Kama ni KE haikuhusu!
 
Wakitoka hapo wana shake hands na wewe, baadavya hapo una nunua vitumbua unakula. Ndiyo maana Tanzania tunapendana sana
Lazima nikushike mkono tu hatupo Japan ila system ya Japan makini Sana unabaki na magonjwa yako no kushikana mikono
 
Mie ndio maana huwa simshiki mtu mkono natoa 5 tuu


Ila sie watoto wa kiislamu tumefundishwa kuikosha tunapomaliza kukojoa na kunawa vizuri.
 
Kustanji kwa mawe matatu..unayatolea wapi
Mawe utayaandaa kabla ya kukojoa. Ni lazima uzingatie baadhi ya mambo kabla ya kukojoa na haifai kukojoa hovyo hovyo si kidini tu bali hata kistaarabu. Usikojoe chini ya mti wa kivuli, usikojoe jalalani, usikojoe pembeni ya shimo wala usikojoe sehemu ngumu ambayo itafanya 'cheche za mkojo kukurukia' mwilini mwako
Kwa faida zaidi juu ya kustanji soma hapa chini

KUSTANJI

Inajuzu/inafaa kustanji (kuchamba) kwa kutumia maji mutlaq (maji halisi) ambayo ndiyo asili katika kujitwahirisha na najisi. Pia inajuzu kustanji kwa kila kitu chenye sifa zifuatazo :

i.Kigumu (kigogofu)

ii.Chenye Kuparuza (kisichoteleza)

iii.Kinachoweza kuondosha najisi.

Vitu vyenye sifa hizi ni kama mawe, karatasi, kitambaa na kadhalika.

Ni vema kustanji, mtu akaanza kwa kutumia mawe/karatasi kisha ndio akamalizia na maji.

Kufanya hivyo ni kwa sababu mawe/karatasi huondosha juta (dhati) ya najisi na maji huondosha athari ya najisi bila ya kuchangayika na juta lake.

Ikiwa atatumia kimojawapo baina ya mawe/karatasi na maji, basi ni bora akatumia maji kwani ndiyo pekee yenye uwezo wa kuondosha juta (dhati) na athari ya najisi, kinyume na mawe na nduguze {karatasi, kitambaa na kadhalika}.

Imepokelewa kutoka kwa Anas Ibn Maalik – Allah amuwie Radhi – amesema :

Mtume wa Allah alikuwa akiingia mahala pa kukidhi haja, mimi na kijana wa rika langu tukimbebea chombo cha maji na fimbo/mkuki mfupi, basi akistanji kwa kutumia maji. Bukhariy na Muslim.

Maelezo : Fimbo/Mkuki ulikuwa ukitumika kama sitara na alama wakati wa kuswali ili mtu asiweze kupita mbele.

Imepokewa na Ibn Masoud – Allah amuwie Radhi – amesema :

Mtume – Rehma na Amani zimshukie – alienda kukidhi haja na akaniamrisha nimletee mawe matatu. Al-Bukhariy.

USISTANJI kwa kutumia najisi nyingine iliyo kavu au kitu kilichonajisika tayari kwani huenda kikaizidisha athari ya najisi badala ya kuipunguza.

Kadhalika ni haramu kustanji kwa kilicho chakula cha binadamu kama vile mkate au chakula cha majini kama vile mifupa. Amesema Bwana Mtume – Allah amshushie Rehma na Amani –

"Msistanji kwa (kutumia) kinyesi cha wanyama wala mifupa kwani hiyo (mifupa) ni chakula cha ndugu zenu majini" Tirmidhiy.

Hakika MWENYEZI MUNGU ANAJUA ZAIDI.


Kustanji kwa mawe matatu..unayatolea wapi
 
Mtoa mada hamkumwelewa lakini pia mlishindwa kumwelewa kwasababu labda amesikia aibu kuweka wazi mambo yake.
Maana yake alitaka tujirekebishe kwa kua akiinyonya husikia chumvi chumvi wakati anapenda sukari.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom