Je hii ni moja ya sababu ya kuachana na mpenzi wako?

kagarara

Senior Member
Nov 23, 2010
118
9
Ndugu wana jf, hv mtu akiwa mtwara na mpenzi wake yuko bukoba na wala hakuna mawasiliano yoyote kati ya hawa wapenzi kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao, je kuna uwezekano wa ndoto zao kutimia walizowekeana? Na je kama ni vigumu, watafanyaje kuhakikisha wanafikia malengo yao mbali na obstacle ya umbali na kutokuwepo kwa mawasiliano?
 
Ukosefu wa mawasiliano unaweza kuchangia wawili kuachana!Ila inategemea sana sababu zinazopelekea hali hiyo na kama wote wanaelewa na wamekubaliana WASIIFANYE hali hiyo kuwa tatizo!Hata hivyo...pamoja na maelewano ni muhimu kama watajaribu na kujitahidi kua na mawasilino baada ya kila muda fulani hivi ili wapate muda wakuongea...kukumbushana malengo yao na kujulishana kwamba bado wapo sambamba!!!Zaidi ya hapo ni utashi wa mtu tu....mnaweza mkalala na kuamka nyumba moja na bado majaribu yakawashinda wao badala ya wao kuyashinda majaribu!!!!
 
Kama wamewekeana mkataba wa kutokuwasiliana hata kama wanazo nyenzo za mawasiliano mf simu, barua, n.k. basi kwa mtazamo wangu, hapo kuna mmojawapo anamlaghai mwenzake. "Usinipigie hadi mimi nikutafute" ni mwanzo wa kutokuwa waaminifu.
 
Dah!
Mawasiliano ndio mpango mzima. Muwe mnatumiana hata barua. Ikifika stand inadondoshwa muhusika anapelekewa na atakayeiokota.
 
Mbona zamani hakukua na sim zaidi ya posta uunganishwe na opareta, au utume barua posta, mtu yuko songea mwingine tarime lakini mwisho wa siku ndoa, tena ya kudum na amani tele why not sasa.
 
mawasiliano ya wapenzi ni tofauti sana. Sio lazima simu itumike na yatadumu tu. Kabla ya kuwepo simu mapenzi hayakuwepo? Je hayakudumu? Siku hizi blah blah nyingi tu kwenye mahusiano
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom