Je, hii ni kweli au uzushi kuhusiana na bei za vocha za simu kupanda bei?

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,918
1,993
Wakuu niko huku a town lakini kuna habari zinaendelea kuenea kuwa utapoenda dukani kununua vocha ya buku itakulazimu utoe buku na Mia au vinginevyo ununue kupitia huduma za simu au kama ni vocha ya tsh 2000 itabidi ulipie 2200,imekuwa wiki nzima nikisikia habari hii na kuna jamaa amenidhibitishia jana amenunua vocha kwa bei la ongezeko.Ninaomba wenye taarifa rasmi mnijuze kama swala hili ni kweli au uzushi
 
Ni kweli na hakika hata arusha
 
Achana na kununua vocha,

Nunua/weka pesa kwa tigo pesa, m pesa airtel money,halopesa na mitandao mingine halafu unga kifurushi au nunua salio
 
Ni muda kidogo tokea zipande, mimi hata sishangai , nitashangaa kuona kitu ambacho hakijapanda bei .
Tunaendelea kuishukuru na kupongeza serikali ya awamu ya sita, wanajitahidi sana.
Kwahiyo kumbe imepanda muda
 
Kwa Sasa nipo hapa vingunguti kwa pelapela dsm kila duka nalo ulizia vocha naambiwa tsh 1200 kwa vocha ya buku na 600 kwa vocha ya jero

Hakika mama anaupiga mwingi sana
Sasa mitandao ya simu iko kimya haizungumzi lolote kuhusiana na mabadiliko haya
 
Ni kweli mkuu

Kwa Sasa nipo hapa vingunguti kwa pelapela dsm kila duka nalo ulizia vocha naambiwa tsh 1200 kwa vocha ya buku na 600 kwa vocha ya jero

Hakika mama anaupiga mwingi sana
Kwa akili kama hizi watauzia vocha ya 500 sh 1000/ nchi imejaaa mazezeta
 
Inawezekana kweli jamaa bado ana mzigo wa zamani,inasikitisha usikii kiongozi yoyote au mamlaka yoyote ikitoa tamko lolote
Nimetoka kununua sasa hivi?nimeuziwa bei ya kawaida ila nimepewa angalizo,kesho bei inapanda,maduka mengine ya jirani yameshapandisha tayari
 
Back
Top Bottom