GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,546
- 108,876
Barua iliyovuja ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Gutterez imesema kwamba kuanzia Mwezi Novemba mwaka huu Umoja huo utakuwa hauna Hela kutokana na kwamba Wanachama wake wengi kutokulipa Ada yao hivyo kuyaweka rehani Maisha ya Wafanyakazi 37,000 duniani kote na Kuathiri Shughuli nyingi kutokutendeka vyema.
Kuelekea Kuumaliza mwaka Umoja wa Mataifa unahitaji Kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 230 ( Tsh Bilioni 23 ) ili kuweza Kuendeshea Shughuli zake na ndizo Hela ambazo mpaka hivi sasa hawajazipata kutoka kwa Bajeti yao ya mwaka ya Dola za Kimarekani Bilioni 5.3 ( Tsh Trilioni 540 ) hivyo Katibu Mkuu huyo anaona kuwa huenda wakashindwa Kutekeleza Majukumu yao ya Kiutendaji.
Kutokana na hali hii ya ‘ Ukata ‘ unaoikumba Taasisi hii muhimu ya Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu huyo amesema ya kwamba imewabidi sasa walazimike kuyaanza Maisha mapya ambayo hawayakuyazoea kwa Kipindi kirefu ( miongo mingi ) ya Kubana Matumizi ambapo na Wao kwa sasa wameanza Kupunguza idadi ya Makongamano na Mikutano yao, Kupunguza Safari za Maofisa wake lakini kama haitoshi wamelazimika pia kuanza Kuwakatia Tiketi za ‘ Economy Class ‘ Maofisa wake badala ya zile za ‘ First Class ‘ ambazo walikuwa wakiwakatia kutokana na Hadhi ya Taasisi hiyo.
Kwa Mtazamo wangu mdogo tu na pengine usio rasmi An Eagle naona kwa ‘ Ukata ‘ huu unaoenda Kuikumba Taasisi hii muhimu ya Umoja wa Mataifa ( UN ) huenda pia ‘ ikawaathiri ‘ kwa Kiasi kikubwa Wanajeshi wetu wengi wa Kulinda Amani waliotapakaa katika nchi kadhaa hivyo kusababisha wengi wao Kulazimika Kurejea nchini na hata wasipate yale malipo makubwa ambayo huwa wanayapata na kupelekea Kusababisha ‘ mitafaruku ‘ mikubwa ndani ya Majeshi yetu au hata katika Serikali zetu kwani kuna Tetesi ( japo bado sijazithibitisha ) kwamba wapo baadhi ya Wanajeshi ambao ‘ huwaonga ‘ Wakubwa zao ili wawepo katika hizo ‘ Missions ‘ hasa hasa kwa nchi kama za DRC na Sudan ya Kusini wakiwa na mategemeo ya kwamba wakirudi huko Umoja wa Mataifa ( UN ) huwa wanawalipa Kiasi kikubwa cha Pesa kuanzia Tsh Milioni 75 hadi hata Tsh Milioni 90 kutegemeana na Makubaliano ya Serikali husika na Bajeti za UN kwa wakati huo.
Hapo juu nimekuja na Mashaka kuwa huenda huu ‘ Ukata ‘ unaoikumba sasa Umoja wa Mataifa ( UN ) ukawa ni aina fulani hivi ya ‘ indirect sabotage ‘ kutoka kwa nchi kama ya Marekani ambayo ndiyo inaongoza kuwa Mchangiaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa ( UN ) ambapo ukiondoa tu Michango ya nchi Wanachama wote duniani wao ( Marekani ) peke yao wanachangia 22% ndani ya United Nations ( UN ) hali ambayo kwa kiasi fulani inawafaya wawe na Sauti ( Kibesi ) dhidi ya ‘ Sekretarieti ‘ nzima ya Umoja wa Mataifa.
Yawezekana Marekani ‘ imechukizwa ‘ ama na Kitendo cha Umoja wa Mataifa kutoonyesha Uungwaji wake mkono kuhakikisha kuwa ‘ Maadui ‘ wakubwa wa sasa wa Marekani kama Iran na Korea ya Kaskazini hawachukuliwi hatua madhubuti kama sehemu ya ‘ Kuwadhoofisha ‘ kusudi hata baadae Marekani akianzia Vita nao ( hizo nchi ) basi aweze ‘ Kuzipiga ‘ Kiurahisi hivyo kuzidi Kujiimarisha Kiuchumi na hata Kimkakati.
Hata hivyo nimeuleta hapa huu Uzi ili ‘ Wajuvi ‘ na ‘ Wabobezi ‘ wa Masuala haya ya Kimataifa nanyi muweze Kuchangia Kiukamilifu na kuweka uzoefu wenu juu yah ii hali ili basi na Sisi wengine akina An Eagle tuweze Kujifunza zaidi kwani hakuna Jambo la Kimjadala ambalo ukilileta hapa JamiiForums litashindwa Kujadiliwa Kimantiki.
Karibuni.
Chanzo Taarifa: Mtandao wa Gazeti la The CITIZEN.