Je Hii ndio ile Filamu ya Mwigulu ya Igunga Tuliyokuwa tunaisubiria?

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Nimekuwa nikifuatilia Mikitano ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba . Huwa anaongozana na Kijana aliyemwagiwa Tindikali Igunga, kisha kupelekwa India na CCM (Ingawa naamini kwa fedha za Serikali). Huyu jamaa amekuwa ni moja kati ya Sera za Mwigulu. Nikimwangaliaga huyu jamaa huwa namuonea Huruma anavyotembezwa Majukwaani na Mwigulu. Najiuliza

1. Hivi hii inamsaidia Mwigulu na CCM kweli?
2. Kwa kuwa waliommwagia Tindikali so far hawafahamiki, na kwa kuwa Mwigulu anatembea na jamaa "Kipropaganda zaidi" , je haoni kwamba inamfanya jamaa badala ya Kuonewa Huruma na Wananchi anaonekana Mpuuzi anayekubali "Kutembezwa" na Mwigulu kipropaganda
3. Does this add any value to CCM Campaign au inazifanya zionekane ni Propaganda?
4. Je huu si Udhalilishaji
5. Any way au tuulize " Jamaa analipwa Kiasi Gani"?
6. Je haitaonekana kwamba CCM wanamganda kada wao ambao inaaminika wao ndio waliomwagia Tindikali ili Watengeze Filamu ambayo Mwigulu anatembea Kuiuza

Mimi nauliza tu kwamba je Ile Filamu ya Mwigulu Igunga ndio imetoka sasa na Jamaa anauza CD kupitia Majukwaa ya Siasa

DSC06895.JPG

Nyingine

DSC06896.JPG

Labda Swali la Kujiuliza "UTU" Is this Guy Comfortable?
 
Last edited by a moderator:
Hii ni udhalilishaji pia kampeni inahusu madiwani wawakilishi wa watu kwenye local govt; lakini kwa huyu mwigulu ni nafasi ya kampeni za kukithiri uovu wake.
 
Nashawishika kudhani kuwa Mwigulu is not ik upstairs. Angalia minguo aliyovaa na hiyo midevu kama savimbi.
 
Labda Swali la Kujiuliza "UTU" Is this Guy Comfortable?
mimi nadhani, kama, Mwigulu anamtumia huyo kijana kutuhumu, basi anakosea.
Mwigulu alipaswa baada ya matibabu kuwapandisha mahakamani watesi wake ambao mwigulu anawatuhumu badala ya kumgeuza 'Agenda/bango' la kampeni zake. Muda si mrefu wataanza kumtembeza mjane wa Mwangosi, hawakawii hawa jamaa.
Huyo kijana anajitambua sana ila atanyaje wakai ana njaa huku kapewa dili la aina hilo lisilo na kutoa jasho.
 
Sijajua mwigulu anamaanisha nn na anataka umma uelewe nn? Huyu jamaa anaratibu mipango ya ovyo ovyo na baadae anawatuhumu wana CHADEMA ,huku nikukosa sera. Nashangaa huyu jamaa anakubali vipi kutembezwa wakati hata aliyemmwagia hamjui
 
Dah Ila Umaskini Mbaya sana

Alijisema Ndugu yangu Chris Lukosi kwamba "Sisi sote ni ndugu adui yetu ni CCM" Wakamshughulikia wakataka Kumnyima Tenda na Kufilisi Kampuni yake Kijana akasalimu amri sasa anataka na sisi tumfuate LoL Njaa ni kama Kidonda cha Tumbo kikikupata ni Lazima Ujikuanyate
 
Last edited by a moderator:
propaganda zakishenz.i sana hizo!anamdhalilisha bure mwadhiriwa wawatu,najamaa njaa inamdhalilisha sana!poor mwigulu......!
 
mimi nadhani, kama, Mwigulu anamtumia huyo kijana kutuhumu, basi anakosea.
Mwigulu alipaswa baada ya matibabu kuwapandisha mahakamani watesi wake ambao mwigulu anawatuhumu badala ya kumgeuza 'Agenda/bango' la kampeni zake. Muda si mrefu wataanza kumtembeza mjane wa Mwangosi, hawakawii hawa jamaa.
Huyo kijana anajitambua sana ila atanyaje wakai ana njaa huku kapewa dili la aina hilo lisilo na kutoa jasho.

Hapo kwenye Blue kaka ni Suala la Muda tu
 
Who is there to tell this Guy( Mwigulu)that we are fade up with him.This type of intimidation can't be accepted.
 
Tatizo la siasa unaumizwa bila hatia yoyote. We angalia mfano mwangosi kwanini CDM wasifungue kesi ikiwa ushaidi wanasema wanao kuwa polisi ndo walifanya vile? Ukitazama wanasheria walioko CDM unabaki unashangaa tuu. Vilevile kwa mwigulu kwanini asiende mahakamani kushtaki hao waliomfanyia ukatiri jamaa?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Filamu itaisha bila watu kuilewa star wa filamu ni nan.na wajue cku ya kufa nyan miti yote huteleza.
 
Tatizo la siasa unaumizwa bila hatia yoyote. We angalia mfano mwangosi kwanini CDM wasifungue kesi ikiwa ushaidi wanasema wanao kuwa polisi ndo walifanya vile? Ukitazama wanasheria walioko CDM unabaki unashangaa tuu. Vilevile kwa mwigulu kwanini asiende mahakamani kushtaki hao waliomfanyia ukatiri jamaa?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

well said...
 
analipwa sh 100,000 kutwa ,kwa kusimamishwa mkutanoni na kusema walionidhuru ni CDM.

siasa hivi nooooma!
 
Tatizo la siasa unaumizwa bila hatia yoyote. We angalia mfano mwangosi kwanini CDM wasifungue kesi ikiwa ushaidi wanasema wanao kuwa polisi ndo walifanya vile? Ukitazama wanasheria walioko CDM unabaki unashangaa tuu. Vilevile kwa mwigulu kwanini asiende mahakamani kushtaki hao waliomfanyia ukatiri jamaa?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Hivi wewe mheshimiwa unaishi sayari yetu kweli? Maana nikiuliza Tanzania itakuwa kama nakuita jiwe lisilo na ufahamu wa kinachoendelea! Ushahidi wa Mwangosi ni wa kutafutwa? Si kuna kesi ya kisanii inayoendelea?
 
Hawa jamaa wanawatisha watanzania bila kuwasaidia kutatua matatizo yao .tuweke pembeni siasa za chuki
 
Tatizo la siasa unaumizwa bila hatia yoyote. We angalia mfano mwangosi kwanini CDM wasifungue kesi ikiwa ushaidi wanasema wanao kuwa polisi ndo walifanya vile? Ukitazama wanasheria walioko CDM unabaki unashangaa tuu. Vilevile kwa mwigulu kwanini asiende mahakamani kushtaki hao waliomfanyia ukatiri jamaa?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
CDM hawana mamlaka kisheria kufungua kesi. Kesi hufunguliwa na mwendesha mashtaka wa serilaki, DPP. Kwenda polisi kupeleka malalamiko ni hatua nyingine, na kufunguliwa kesi ni hatua nyingine. Umesahau kuwa CDM walipeleka mashtaka polisi dhidi ya Rage kumshambulia na kumjeruhi kiongozi wa CDM Dodoma, lakini hadi leo jalada lipp kwa DPP na hakuna kesi iliyofunguliwa?!!!
 
Yani huwa nikiwaza mbinu wanazotumia kina Mwigulu na Nape kuendesha propaganda, natamani CCM itoke tu madarakani walau ikapate nafasi ya kujipanga, maana hawa jamaa wanaiua...
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom