Je hii inaingia kwenye kosa la Human Trafficking kwa sheria za Tanzania?


Brooklyn

Brooklyn

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Messages
1,461
Likes
58
Points
145
Brooklyn

Brooklyn

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2009
1,461 58 145
Wadau wa sheria nina swali nataka msaada wa kisheria.

Kuna mtu kanitoroshea binti wangu wa kazi na kwa bahati nzuri katika pitapita za vijana wangu hapa mjini wakafanikiwa kukutana naye. Baada ya kumbana na maswali wakitaka kujua sababu iliyomfanya aondoke bila kuaga, binti akajibu kuwa alishawishiwa na mmoja wa jirani zetu hapa mtaani.

Akaendelea kusema kuwa yeye hakupenda kuondoka ila aliahidiwa ahadi kem kem ndo maana akaamua atoroke. Binti akasema anaomba arudi nyumbani kwani maisha ya huko alikoenda sio mazuri kwa upande wake na ananyanyaswa sana na bosi wake wa mpya.

1. Nataka kujua naweza kumfungulia mashtaka huyu jirani yangu kwa kunitoroshea binti wa kazi bila ridhaa yake (human trafficking)?

2. Katika kesi hiyo naweza pia kudai fidia ya gharama nilizogharamia kumleta hapa mjini huyu binti na compensation zingine?

Natanguliza shikrani wana JF.
 

Forum statistics

Threads 1,274,330
Members 490,664
Posts 30,508,558