Je hifadhi ya barabara ni umbali gani toka barabara husika?

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,322
29,583
HABARI.
Nimekuwa nikisikia watu ktk mazungumzo kuwa hifadhi ya barabara ni mita 120, wengine 60 na wengine na namba zao ilimradi tu kila mtu kasema lake.
Je hifadhi ya barabara ni umbali gani toka barabara husika na hicho kipimo ni kianzia upande mmoja au ni pande zote mbili?? Namaanisha, kwa mfano unaposema mita 120 hizi ni zinagawanywa nusu 60 upande mmoja na nusu myingine 60 upande wa pili au ni upande mmoja tu yote 120? Na je, huo umbali unaanzia kupimwa katikati ya barabara au kwenye kingo za barabara??
 
Mara nyingi swali hili huwa linajibiwa sana na wanasiasa badala ya wataalamu kutoka Idara za UUM. Pamoja na kuwepo kwa vigezo kwa mahsusi kwa kila barabara wahusika huwa hawatoi ufafanuzi hata pale inapotoshwa. Nijuavyo mimi ni kuwa ardhi inayokadiriwa kujengwa barabara kama ile ya Morogoro ina upana wa mita 120.

Barabara inatakiwa ijengwe katikati ya mita hizo 120/2 ambayo ni mita 60. Kuanzia katikati unapata mita 60 kila upande ambapo hujumisha nusu ya barabara lengwa,barabara ya matengenezo,wapanda baiskeli na waenda kwa miguu na pembeni kabisa nguzo za umeme simu na reserve yenyewe. Natumaini tutapata mtaalamu wa kutoa ufafanuzi zaidi.
 
Daaa.., huu Uzi unaweza kuliza Watu upya, ukute Mtu ameshakubali M 30, akisoma hapa anaambiwa eti bado yupo road!!!
 
HABARI.
Nimekuwa nikisikia watu ktk mazungumzo kuwa hifadhi ya barabara ni mita 120, wengine 60 na wengine na namba zao ilimradi tu kila mtu kasema lake.
Je hifadhi ya barabara ni umbali gani toka barabara husika na hicho kipimo ni kianzia upande mmoja au ni pande zote mbili?? Namaanisha, kwa mfano unaposema mita 120 hizi ni zinagawanywa nusu 60 upande mmoja na nusu myingine 60 upande wa pili au ni upande mmoja tu yote 120? Na je, huo umbali unaanzia kupimwa katikati ya barabara au kwenye kingo za barabara??
swali zuri sana kijana
 
Back
Top Bottom