Je, HESLB ina mchango katika kutokomeza umaskini?

sabuwanka

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
690
751
Wanabodi, poleni na majukumu pamoja na misiba iliyowakuta wenzetu wa moshi baada ya kukanyagana wakati wakati wakikanyaga mafuta ya upako chini ya neno la unabii kutoka kwa mtumishi mwamposa mnamo 01.02.2020

Pili, naendelea kupongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa kuongeza utoaji wa mikopo kwa vijana wa elimu ya juu, sambamba na hilo serikali hii ndiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kusimamia urejeshwaji wa mikopo kwa wanufaika hasa waliohitimimu kwa wingi 2009-2019, hili ni jambo la kupongeza!

Lakini pia kumekuwa na vilio kwa wanufaika walioajiriwa sekta za umma na binafsi juu ya urejeshwaji wa mkopo kwa 15% kwa mwezi toka katika bisic salary zao na tozo mbali mbali zinazoambatana na urejeshwaji wa mkopo huo,

Hivyo napenda wadau kwa ujumla tujadili zoezi hili la ukopaji, na urejeshwaji wa mkopo , je limesaidia kwa kiwango kikubwa kutokomeza umaskini ?hasa kutoa fursa kwa wengine kukopeshwa zaidi?

Mwisho kabisa natoa tahadhari kwa wanufaika wa sasa watumie mikopo kwa uangalifu maana kinachokopeshwa kwa mwezi ni sawa na mshahara utakaopata baada ya kuhitimu kwa mwezi, achilia mbali muda utakaotumika kurejesha deni hilo.

Karibuni
 
Walininyima mkopo hawa jamaa. Maisha yalikua magumu mtaani, saivi nakunja mpunga naweka kiunoni nasepa zangu
 
Bodi hii hii ya mkopo ambayo inawakata watu ambao hawajawah hata kusoma degree. Mtu kaishia form four Bodi inamkata hela yake. Bodi mnawasumbua vijana. Basi watafitieni na Vyeti vya digrii bhas
 
Uzi makini sn.Nazani bodi ya mkopo ni janga kubwa kwa atakaeajiliwa serikalini lakn kwa waliokosa kazi na waliojiajiri szani km kwao ni janga.

Sent using Jamii Forums mobile app
JPM kafanya juhudi kuwatafuta walioajiriwa katika sekta rasmi....lakini pia kadri unavyochelewa kulipa deni ndo linaongezeka!!!! Siku wakitumia wakusanya madeni hata wasikuwa na ajira watabainika
 
Bodi hii hii ya mkopo ambayo inawakata watu ambao hawajawah hata kusoma degree. Mtu kaishia form four Bodi inamkata hela yake. Bodi mnawasumbua vijana. Basi watafitieni na Vyeti vya digrii bhas
Da haya nayo nayasikia sikia ila sio kwa sauti kubwa
 
Back
Top Bottom