Je Hazina Walikuomba Kibali cha Semina M. PM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Hazina Walikuomba Kibali cha Semina M. PM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichankuli, Dec 23, 2008.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2008
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Jana niliona kwenye taarifa ya habari watumishi wa Hazina wakiwa kwenye semina kule Bwagamoyo. Ni majuzi tu Kiranja Mkuu wa Serikali Bungeni alikoroma kwamba semina zote lazima atie baraka zake ndipo ziendeshwe. Sasa sijui kama hawa jamaa wanaokaa na fedha za nchi nzima (zikiwemo zinazosazwa kwenye bajeti za nyuma) walipeleka maombi ya kupata kibali cha Mr. PM. Lakini kuna maswahi kadhaa ambayo yanakizonga kichwa changu juu ya mkwara huu:

  1: Umma utakuwa unajuwaje kwamba Mr. PM ametoa baraka za kufanyika kwa semina fulani?
  2: Mafungu ya kuendesha semina, wekshopu na makongamano haya yalishaidhinishwa na Bunge ambalo Mr. PM ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za serikali ndani yake. Sasa kukataza semina zisifanyike siyo kukiuka maazimio ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano?-Hapa unaweza kujumuisha na ununuzi wa Mashangingi (sitetei ila naonyesha jinsi ambavyo hii inaweza kuwa danganya toto)
  3: Lakini kingine kinachojitokeza hapa ni kwamba inaonyesha kwamba wabunge wetu (hasa wa chama Twawala ambao ndiyo huunga mkono kwa asilimia 100) huwa hawasomi kwa makini michanganuo ya bajeti katika kamati zao za Bunge. Je yawezekana pia na Mh. PM naye huwa hasomi na kujua kwamba kwa mwaka fulani wizara fulani imeweka bajeti ya kuendesha semina kadhaa?
   
Loading...