Je, Hayati Rais Magufuli alikuwa ni mtu wa namna gani hasa?

Achanakia

Member
Jan 28, 2021
70
81
Je, unaweza kumwelezea Hayati kama alikuwa ni mtu wa namna gani?

Wakati wa uhai wake kwenye vyombo vyote vya habari ukiacha mitandao ya kijamii, magazeti na television, na hata vijiweni ilizoeleka kusikia sifa nyingi positive kumhusu yeye.

Kwenye mitandao ya kijamii kidogo kulikuwa na watu wachache walikuwa wanaweza kuandika post zinazoelezea neative kumhusu Hayati. Hao walihakikisha hawatumii majina yao halisi katika kupositi hizo negativity, wachacha waliokuwa wanatumia majina halisi ni wale ambao walikuwa radhi kwa lolote.

Kabla ya Hayati, kwenye utawala wa JMK ilikuwa ni kawaida kabisa kuona watu kwenye vyombo vya usafiri, vijiweni, kwenye vyombo vya habari vyote zikiwemo tv n.k. watu walikuwa huru kuongea na kutoa mitazamo yao kuhusu Rais na serikali kwa ujumla tofauti na kipindi cha Hayati ambapo watu walikuwa huru kuimba sifa njema tu.

Baada ya kifo chake kumetokea pande mbili zinazokinzana. Upande mmoja umejikita katika kuanika ubaya wa Hayati na Upande mwingine unatumia nguvu nyingi kukanusha na kuelezea mazuri ya hayati kwamba alikuwa mtu mwema na aliyefanya maendeleo makubwa haijapata kutokea katika historia ya nchi yetu.

Upande huu unawalaani sana wale wote wanaosema ubaya wa Hayati kwa kuwaona kama hawana shukrani na sio wazalendo kwa nchi na kwa Hayati. Wanaenda mbali zaidi kwa kutamani wote wanaomsema hayati kwa ubaya kama ingewezekana serikali iwakamate na kuwapa adhabu kali sana. Hiyo kama haitoshi kundi hili limefika mahali linakihusisha kifo cha Hayati na njama, kwamba Hayati ameuliwa na wabaya wake ambao hawakufurahishwa na misimamo yake kuhusu raslimali za nchi, na pia walikuwa wanamuonea wivu kwa maendeleo makubwa aliyoyafanya kwa muda mfupi.

Mbaya zaidi wanadiliki kuwataja kwa majina hao wanaowaita wabaya wa Hayati.

Kwangu mimi jambo hili halina afya hata kidogo kwa mustakabari wa amani yetu. Maana hili linabomoa zaidi kuliko kujenga. Kwasababu haifai kuwatuhumu watu bila ushahidi.

Sasa katika makundi haya mawili hakuna kundi hata moja ambalo watu wake wanaweza kuelezea mazuri na mabaya ya Hayati kwa pamoja ili tuweze kupima kwenye mizania tupate jibu linaloweza kutuambia Hayati alikuwa ni mtu wa namna gani.

Je, wewe Mwanajukwaa ulivyomfahamu Hayati kwa mazuri na mabaya yake unadhani alikuwa ni mtu wa namna gani?
 
Kwaiyo wanaomuandika vibaya wanatumia nguvu kidogo ila wanamtetea na kumwandika vizur wanatumia nguvu nyingi? Sawa hamna shida lakink tutakutana humu baada ya miaka kadhaa mbeleni.
 
Mimi sina shida na mazuri aliyoyafanya/yaliyofanyika kipindi chake, kwa vile ndiyo kazi tuliyompa na tulishamlipa mshahara.

Tatizo ni yale mabaya aliyofanya yeye binafsi, au na watu wengine ambapo yeye alikuwa kiongozi mkuu.

Kwa sababu hiyo alikuwa ni mtu mbaya sana.
 
Mimi sina shida na mazuri aliyoyafanya/yaliyofanyika kipindi chake, kwa vile ndiyo kazi tuliyompa na tulishamlipa mshahara.
Tatizo ni yale mabaya aliyofanya yeye binafsi, au na watu wengine ambapo yeye alikuwa kiongozi mkuu.
Kwa sababu hiyo alikuwa ni mtu mbaya sana.
Ulivyopigwa chini kwa cheti feki ungefanya QT sasa hivi ungekuwa umeshafika university second year!
 
... mzee wetu, Jiwe, aliamini kwamba ofisa au kiongozi kukaa ofisini ni uvivu!
... hivyo viongozi wote waliokuwa chini yake walifanya kazi kama vibarua wa mtaalam mmoja, YEYE! ... yaani kutwa kucha field na majukwaani na kazi ya ofisini tupa kuleee,
... ALL PLANNING BY ONE BRAIN, JIWE'S, ... means if Jiwe gives garbage then all goes garbage!
PATHETIC!
 
Mheshimiwa raisi Magufuli alikuwa mtawala na kiongozi mahiri katika kusimamia utekelezaji wa yale aliyoyaamini lakini kwenye siasa na diplomasia nadhani alitetereka kidogo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom