Je, Hayati Magufuli alichukia wawekezaji au alichukia wawekezaji janja janja?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,474
8,692
Kwa kumbukumbu zangu Mwendazake hakuwahi kuchukia wala kuwakataa wawekezaji; nakumbuka aliwahi kuwaambia watu wa Mazingira kwamba wanapaswa kufanya uchambuzi wa kimazigira wakati tiyari mwekezaji anaendelea na kazi.

Mwendazake aliwachukia wawekezaji wajanja ambao nazani ndo wengi sana nchi hii.

Hawa hawa tunaoenda kuwapigia magoti wengi ni wajanja janja sana tena mno.

Fikiria Shule ya English Medium ya mwekezaji wa Kikenya inakuwa hadi na Mwalimu wa somo la Kiswahili kutoka Kenya.

Kuna International school pia iko Arusha sitaitaja jina nilichoka kukuta Mwalimu wa somo la Kiswahili ni Mkenya asieee fikiia hapa.

Hawa ndo mwendazake alikuwa anawachukia sana, na ndo mama anataka kuwakumbatia.

Ila kwa kumbukumbu zangu Magufuli hakuwahi kukataa wawekezaji bali wawekezaji wajanja.
 
Kuiba pesa za wafanyabiashara kwa nguvu na kutumia mtutu wa Bunduki,au kubambikia watu kesi za kuhujumu uchumi,ndio kupenda wawekezaji?Rejea hotuba ya Mhe Raisi siku anahutubia Ikulu,alitoa kisa kimoja alichokishuhudia kama Makamu wa Raisi.

Sasa kama Makamu wa Raisi alifika pointi,akashindwa,ndio ujue Jiwe alikuwa mwizi tu,wafanyabiashara aliowapenda ni wale shemeji zake wa Mayanga Co ltd.
 
Inawezekana pia hujui.

Kenya au wakenya wanaongea kiswahili fasaha kuliko sisi.Kwa lugha nyingine Wakenya wanafaa katika somo lakiswahili.

Leo hii ukiweka mtihani wakiswahili Kati ya mwanafunzi wa Kenya na Tanzania.

Mkenya anapata maksi nyingi kuliko Mtanzania.
 
Kwa kumbukumbu zangu Mwendazake hakuwahi kuchukia wala kuwakataa wawekezaji; nakumbuka aliwahi kuwaambia watu wa Mazingira kwamba wanapaswa kufanya uchambuzi wa kimazigira wakati tiyari mwekezaji anaendelea na kazi...
Watanzania waache kulalamika bali wajitume kwa juhudi na MAARIFA kuonyesha utaalamu na umahiri wa kutenda kazi ili wathaminiwe.
 
Je Dangote ni muwekezaji mjanja mjanja?mbona na yeye alitaka kufungasha vilango?alifikia kipindi akasema hadharani kuwa hii nchi hata haieleweki leo anakuja huyu, anatoa maelekezo haya, unayafanya kesho anakuja mwingine tena anakwambia mengine, hata unashindwa ufuate lipi uache lipi?!!na yeye kosa lake kubwa lilikuwa kudai apelekewe gesi kama walivyokubaliana wakati wa kutiliana mkataba, wakamwambia asinunue makaa ya mawe toka Afrika kusini, haya akakubali basi akaanza kuagiza hayo makaa ya mawe toka mto chuma, na liganga akiagiza tani 2000, wanamletea tani 200!!kuwa ndio iliyopatikana tena baada ya muda mrefu!!huwezi ukamlazimisha muwekezaji anunue malighafi nchini wakati hazipatikani kwa kiwango kinachohitajika.shirika la ndege la fastjet nini kililikuta akafikiria kuwafukuza ndio atafanya biashara kirahisi,?
 
Inawezekana pia hujui.

Kenya au wakenya wanaongea kiswahili fasaha kuliko sisi.Kwa lugha nyingine Wakenya wanafaa katika somo lakiswahili.

Leo hii ukiweka mtihani wakiswahili Kati ya mwanafunzi wa Kenya na Tanzania.

Mkenya anapata maksi nyingi kuliko Mtanzania.
pumba,labda wa kenya wa mombasa kidogo wanajitaidi,hiyo ya mkenya kufaulu kiswahili zaidi ya mtz ni kamba
 
Wewe huwajui Wakenya mkuu, nazani uko huko Nanyamba mtwara huwajui,

Badala ya ww kufungua shule, unazunguka kwenye shule walizofungua wakenya kuangalia waalimu wa kufundisha kiswahili! Nyie waswahili mkipata hela mnajenga guest houses, na nyumba za kupanga, kisha wakenya wakijenga shule mnajifanya wazalendo kuangalia waalimu. Ww zungukia short time kwenye guest zako, sio waalimu wa kiswahili kwenye shule ya mkenya.
 
Wewe huwajui Wakenya mkuu, nazani uko huko Nanyamba mtwara huwajui,
Ukifanya interview kishindani na kihalali kabisa kwenye soko la ajira wakenya wengi wako vizuri kulinganisha na watanzania. Tanzania ikithubutu kufungua milango ya labour force kutoka nchi nyingine za East Africa, watanzania wengi hawawezi kushindana na wakenya.
 
Kwa kumbukumbu zangu Mwendazake hakuwahi kuchukia wala kuwakataa wawekezaji; nakumbuka aliwahi kuwaambia watu wa Mazingira kwamba wanapaswa kufanya uchambuzi wa kimazigira wakati tiyari mwekezaji anaendelea na kazi.

Mwendazake aliwachukia wawekezaji wajanja ambao nazani ndo wengi sana nchi hii.

Hawa hawa tunaoenda kuwapigia magoti wengi ni wajanja janja sana tena mno.

Fikiria Shule ya English Medium ya mwekezaji wa Kikenya inakuwa hadi na Mwalimu wa somo la Kiswahili kutoka Kenya.

Kuna International school pia iko Arusha sitaitaja jina nilichoka kukuta Mwalimu wa somo la Kiswahili ni Mkenya asieee fikiia hapa.

Hawa ndo mwendazake alikuwa anawachukia sana, na ndo mama anataka kuwakumbatia.

Ila kwa kumbukumbu zangu Magufuli hakuwahi kukataa wawekezaji bali wawekezaji wajanja.
Watanzania wanaotazama masuala kwa umakini ni wachache. Wengi wetu tunasukumwa na ushabiki yaani "Bendera fuata upepo". Ndio shida yetu kubwa.
 
Kwa kumbukumbu zangu Mwendazake hakuwahi kuchukia wala kuwakataa wawekezaji; nakumbuka aliwahi kuwaambia watu wa Mazingira kwamba wanapaswa kufanya uchambuzi wa kimazigira wakati tiyari mwekezaji anaendelea na kazi.

Mwendazake aliwachukia wawekezaji wajanja ambao nazani ndo wengi sana nchi hii.

Hawa hawa tunaoenda kuwapigia magoti wengi ni wajanja janja sana tena mno.

Fikiria Shule ya English Medium ya mwekezaji wa Kikenya inakuwa hadi na Mwalimu wa somo la Kiswahili kutoka Kenya.

Kuna International school pia iko Arusha sitaitaja jina nilichoka kukuta Mwalimu wa somo la Kiswahili ni Mkenya asieee fikiia hapa.

Hawa ndo mwendazake alikuwa anawachukia sana, na ndo mama anataka kuwakumbatia.

Ila kwa kumbukumbu zangu Magufuli hakuwahi kukataa wawekezaji bali wawekezaji wajanja.
Mfu shetani mtu Magufuli alikuwa anataka mwekezaji atakayekubali kufanya naye ufisadi vinginevyo anakufilisi na kukufungulia kesi ya kutakatisha fedha na uhujumu uchumi!
 
Wakati unazuia Mkenya kuleta mwalimu wa Kiswahili, Je sheria za nchi yako zilikuwa zinamruhusu kufanya hivyo au la?
1620310317286.png

Sijui kama hiyo extract ya Non-Citizen(Employment Regulation)Act, No 1 ya 2015 inajibu swali lako…Section 11(2).
 
Kwa nini kila "move" anayoifanya Mama kuna njema zinakuja kutetea ya "mwendazake". Kwani kipi kinawauma?
Mzee Mwinyi aliingia na "Ruksa yake", akatandika "reforms" za nguvu, tena nyingine zilizokuwa tofauti na mtazamo wa Nyerere. Lakini hadi leo jina lililo midomoni ni Nyerere. Legacy huongea yenyewe, haitetewi!
 
Back
Top Bottom