Je, haya ya Faru John, Fausta sasa Vicky ni mfumo mpya wa wapigaji?

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
7,907
13,367
Habari wandugu

Nitaenda moja kwa moja kwenye maelezo yangu kidogo sababu hili ni swali wenye majibu watujuze au wachangiaji wengine wachangie zaidi.

Kumekuwa na utaratibu ambao sasa umeonekana kuwa kawaida au mazoea kuwachukua wanyama pori Faru na kuwaweka sijui niite kwenye mabanda ya malezi au Zuu (Zoo)

Kuna taarifa za kuwepo Faru anayeitwa Faru Vicky anayetarajiwa kuwekwa kwenye banda la faru aliyefariki Faru Fausta kwa kile kilichodaiwa ni kumlinda dhidi ya maadui (wanyama wenzake) ambao si majangili.

Hili linanifanya nijiulize huu utaratibu/mazoea ni dili la mtu/watu au kuna sheria inatutaka kufanya hivyo?. Sababu ni gharama sana kuhudumia faru hawa wakiwa katika mfumo huu wa vyumba vya malezi huwenda ikawa ni gharama kuliko hata kuongeza askari wanyama pori wakapambane na ujangili.

Mtazamo wangu hili tuliangalie upya, huwenda tunatumia gharama kubwa bila msingi wowote hasa ikizingatiwa kumetolewa sababu ya eti ni mzee wa miaka 49 hivyo analindwa dhidi ya wanyama wenzake. Kwanini tusiache mfumo wa asili ufuate mkondo kisha sisi tukajikita kupambana na majangili?.

Nasikitika swali langu halijawa fupi kamanilivyo ahidi hapo awali na huwenda limegeuka makala fupi.

Shukrani.


VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA
 
Kwa uelewa wangu nikuwa wanawekwa kwenye hiyo sehemu maalumu kulinda asidhuriwe na wanyama wakali maana nguvu za kujikinga kupigania uhai wake hana kama zamani. 2 nikwaajili pia ni kati ya wanyama wanao pungua kwa kasi sana Duniani, huwezi kuta swala au pofu wakahifadhiwa hivyo labda iwe kunatafiti maalumu inafanyika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom