Je? Haya majukumu ya Makamu wa Rais anaagizwa na Rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je? Haya majukumu ya Makamu wa Rais anaagizwa na Rais?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zipuwawa, Apr 21, 2012.

 1. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  47.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa
  ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya
  Muungano kwa jumla, na hususan-
  (a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku
  hata siku za Mambo ya Muungano;
  (b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
  (c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini
  au yuko nje ya nchi.

  Je haya majukumu ya Makamu wa Rais Yeye kuwa wa Kutembea na mikasi na Kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo na hata mashule , hospital, na huduma za maji hata kama hazijakamilika. Makamu wa rais Toka ateuliwe yeye amekuwa akitembea tu kufungua miradi mbalimbali hata kama haijakamilika Je hizi ndizo kazi alizo tumwa au kuagizwa na Rais?
  Je viongozi wetu wanafuata katiba? Makamu wa Rais tumeshuhudia toka aanze kazi amekuwa akitembea na mikasi akiwa na Msururu wa Magari kwa kwenda kufungua miradi ambayo ingeweza hata kufunguliwa na wakuu wa mikoa au wilaya. Nauliza huu si ufisadi mwingine kwa gharama kubwa za misafara ya Ndani isiyokuwa na Tija?
  Je wamekubaliana na rais kuwa makamu awe wa kuzunguka nchi nzima na Rais kuzunguka Dunia nzima? Tuangalie leo hii hali ya nchi migogoro ni mingi lakini Rais na Makamu wake wapo kwenye safari zisizokuwa na tija.

  Ni bora tuiangalie katiba yetu inayowabeba watawala kwa kuendelea kuwaburuza tumeona jana Spika wa Bunge akizungumzia Katiba je haya ya Viongozi wa juu hawaijui katiba? au katiba ni kwaajili ya kuwabana watawaliwa tu?
   
 2. k

  kubane Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umeongea point sana bro, akistaafu atakuwa fundi kushona, haiwezekani m2 kila siku misele tu. tena wote wawili aisee, naona hawa hata briefing hawapeani ase.
   
 3. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Haiwezekani makau Wa Rais yeye kuwa Mtu wa Misele ya Ndani isiyokuwa na tija na msururu wa magari unaotia hasara nchi yetu
   
Loading...