Je, hawa wateule wa Rais ni sheria zetu butu, uzembe au?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
JE, NI SHERIA BUTU, UZEMBE AU NI MAZOEA?

Na Elius Ndabila
0768239284

Nikitazama mchakamchaka wa watumishi pale tu Mkuu wa nchi anapotoa maagizo ninabaki kujiuliza je ni sheria zetu butu, je ni uzembe kwa watu ambao Mh Rais amewaamini kumsaidia kusimamia au ni mazoea ya viongozi wetu kuzoea kusukumwa sukumwa?

Yapo matukio mengi ambayo yananifanya nijiulize maswali haya na kushindwa kupata majibu fasaha ya kile ninachokiuliza. Naona Kama Mh Rais ana mzigo mkubwa na kushindwa kufurahia nafasi yake ya Urais kwani muda wote anaumiza akili. Kabla sijazungumza jambo la Dar es Salaam ambalo linabeba headline nyingi ya vyombo vya habari, ninaomba nitoe mifano michache kama rejea kuelekea kujenga hoja zangu za je ubutu, uzembe au mazoea?

Miaka michache iliyopita Mh Rais baada ya kilio cha muda mrefu cha wakulima wa Korosho katika mikoa ya kusini aliwaagiza Waziri Mkuu na Waziri wa Kilimo kuhakikisha wanatatua changamoto za Wakulima hao. Hakika kwa kipindi chote cha Uwaziri wa Kilimo Mh Hasunga alikuwa anashinda mikoa ya kusini hadi kupelekea watu wengine kumtania kwa kumuita Waziri wa Korosho. Mh Hasunga ambaye baada ya kupata Uwaziri sisi watu wa nyanda za juu kusini tulitegemea ndiye atakuwa mkombozi wa zao la Pareto ambalo kwa kiasi kikubwa Wakulima wananyanyaswa kwa kupangiwa bei na kuto kuruhusu Soko huria kwa Wanunuzi. Lakini Hasungu alianzia Mtwara na akamilizia Mtwara. Inawezekana bila Rais kutoa maagizo pengine asingeitwa waziri wa Korosho.

Kama hujanielewa hapa usikate tamaa, mpaka kufika mwishoni utakuwa umenielewa. Mwaka Jana Mwishoni baada ya Mh Waziri Mkuu kuzunguka nchi Nzima aligundua kuwa kuna upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa. Waziri Mkuu aligundua kuwa akiwaachia watumishi wakienda likizo kunauwezekano mkubwa watoto wengi wasipate sehemu ya kusomea. Waziri Mkuu aliagiza watumishi wote kusitishiwa likizo na badala yake wabaki wakishughulikia changamoto hizo. Wakati Waziri Mkuu akitoa maagizo hayo niliandika kwenye makala yangu moja kuwa Je, hii kazi ilitakiwa mpaka Waziri Mkuu aone?

Je, DEDs wako wapi? DCs wako wapi? RASs wako wapi na RCs wako wapi? Je hawa walishindwa kufanya approximate ya ni Wanafunzi wangapi Wataanza darasa la kwanza na kidato cha kwanza mwaka 2021? Hawana data? Kwa sababu niliamini wangekuwa na data basi vyumba vya kupokea Wanafunzi wa mwaka 2021 vingeanza kujengwa tangu mwaka Jana mwezi may. Lakini walisubiria mpaka Mh Waziri Mkuu atoe maagizo. Na kwa taarifa yenu vyumba vinavyojengwa sasa kukimbizana na muda havina ubora kwa kuwa kanuni nyingi za ujenzi lazima zitakiukwa ikiwepo nzege kukaa muda Fulani kabla ya tofali.

Juzi hapa Mh Rais ametoa maagizo tena baada ya clip ya watoto wa Ubungo wanaosoma nje kuvuja. Sitaki niingie sana kwenye undani wa hili kwa kuwa niliandika mawazo yangu juu ya UZEMBE huo. Lakini ninachotaka kuandika hapa ni kuwa baada ya tamko la Mh Rais tumaona picha mbalimbali za hiyo shule zikatimia na vyombo vya habari na viongozi kadhaa wa Dar Es salaam wakiendelea na ujenzi. Mimi nimetafsiri hizo picha Kama Kejeri au Kama kuomba msamaha kwa Mh Rais kuwa tumetii agizo au Kama maonyesho. Nimejiuliza kwa mkoa wa Dar es salaam ni shule hiyo tu yenye matatizo hayo? Shule zingine hazipo? Au wanataka clip zitembee za shule zingine ili tena hamishie drama huko? Nilikuwa ninadhani hiyo ya Ubungo ingetumika kama picha tu, lakini ingewafanya viongozi wawe busy Wilaya zote. Kama wapo busy Wilaya zote kwa nini picha zingine hatuoni? Au mpaka yatoke maagizo mengine?


Wakati haya yanatokea ninapata shida, kwa nini viongozi wa huku chini wanashindwa kufanya kazi ambazo ni majukumu yao wanasubiria mpaka viongozi wa Taifa watoe maagizo? Je kuna tatizo katika sheria zetu katika kujenga dhana ya uwajibikaji? Je Kama ni UZEMBE wanaopewa nafasi hizi hawana sifa za kuwa hapo walipo na ndiyo maana wanasubiria maagizo?

Taifa linahitaji kujenga uwajibikaji. Kama tatizo ni sheria tunatakiwa kuzifanyia marekebisho sheria zetu ili kila mtu ajue majukumu yake. Inawezekana ni ubutu wa sheria zetu ndio unawafanya watu kulala au ni usimamizi.

Leo hii ninaandika mafuta ya kula yamepanda bei Mara dufu. Kupanda bei kwa mafuta ya chakula yameenda kuathiri moja kwa moja bei ya vyakula mahotelini, Migahawani na kwa Mama ntilie. Sidhani Kama Waziri wa viwanda ameshatoa kauli ya kwa nini mafuta yamepanda bei. Sijamsikia. Je hili nalo linasubiria Rais au Waziri Mkuu aseme ndipo Waziri wa Viwanda aingie kufanya msako wa mafuta? Rais MAGUFULI anatamani kutuachia Tanzania tukiwa Kanani, Lakini baadhi ya Wasaidizi wake wanatamani kutuona tunaendelea kuishi Misri.
 
Dawa no kuanzishwa kwa ukurasa maalumu utakao kuwa una onesha video clips za ubovu wa shule nchi nzima
 
JIBU NI JEPESI MBONA...

THIS IS A CENTRALIZED REGIME...

Hao wateule wanadance according to the beat...

Unaweza ukajifanya mbunifu kufanya jambo zuri sana mbele ya jamii, ila mbele ya MKUU Ukaonekana umefanya upuuzi mkubwa sana...kwa sababu UBUNIFU WAKO HUJAANZIA KWA MKUU...
 
Mtukufu amechukua mapato yote kuacha manispaa choka mbaya, kila kitu anacho yeye ndio mpiga ngoma muanzisha wimbo na mchezaji yeye wewe uige anavyotaka.
 
Back
Top Bottom