Je, hawa waliotumbuliwa na kupelekwa mahakamani, ndo Mafisadi tunaoambiwa wamefikisha taifa hapa lilipo?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Heshima kwenu wakuu,

Sasa rais Magufuli ana miaka Miwili, je tutegemee mafisaidi waliofanya nchi yetu kuwa masikini kukamatwa au ndo hawa wa vyeti feki na watumishi hewa?

Magufuli ana Jeshi, Polisi, takukuru na TISS na ndani ya miaka miwili kashindwa kutuonesha hao mafisadi, je tumpe miaka mingapi ili atuoneshe?

Kwenye miaka Miwili amejitahidi kuonesha uwezo wake na nguvu za hali ya juu na weledi wa kiwadhibiti Wapinzani kuongea na kuanzishwa kwa vyama vya siasa. Je anaposema mafisadi waliofanya nchi kuwa masikini anamaanisha Siasa za Wapinzani?

Kwanini amehamishia gia angani ya kupambana na mafisadi, wauza dawa za kulevya badala yake kawekeza kwenye kupambana na wanaomkosoa?

Hadi leo sijaona fisadi aliyekamatwa, naona wanakamata Vijidagaa. Tuliambiwa Lowassa fisadi, kwanini anaogopwa? Akamatwe akanyee debe.

Vitisho vya Watawala vya kuongea kwa kufoka huku wamekunja sura hakutatuondoa kwenye Umasikini wala mkwamo wa kitaifa.

Nlienda Mahakama ya Ufisadi iliyopo katika Shule Kuu ya Sheria, pembeni mwa kituo cha mabasi cha Simu 2000, Ubungo Dar es Salaam nimekuta nyasi zimeota mlangoni, hamna kesi wala mashauri. Milango ipo wazi na hakuna kazi zinaendelea. Aibu, tanzania haina mafisadi?

Watanzania tuwe na mjadala wa kitaifa kujua tutajikwamuaje hapa tulipo.

Je hawa walioshughulikiwa ndio mafisadi au tutegemee wengine? Miaka miwili tumemshindwa hata fisadi mmoja? Eti tunakamata mwanamke anaeonekana kuishi kitajiri. Kafunguliwa mashitaka ya kuishi kifahari. Hahaaaaa...

Afisa msaidizi wa Forodha TRA, Jennifer Mushi afikishwa Mahakamani kwa kumiliki magari 19 na kuishi maisha ya kifahari
 
Back
Top Bottom