Je, hatuwezi kuwa na mchunguzi huru humu nchini mwetu?

Wellwell

Member
Jun 27, 2012
20
4
I salute you guys (Wana JF) kwa michango yenu yenye busara, positive thinking na ya kuelimishana.

Baada ya kufikiria sana juu ya matukio ya kusikitisha sana kama yale ya Mbeya kwa kuuawa Mwangosi, mauaji ya Arusha, Zanzibar, Morogoro na sehemu zinginezo nyingi tu, nashindwa kuelewa taarifa za uchunguzi wa matukio hayo. Sijui kama kuna mtanzania mzalendo wa dhati anayeweza kusema kuwa aliridhika na taarifa za uchunguzi wa matukio hayo. Au anaridhishwa na mfumo unaotumika kuchunguza matukio hayo.

Je, hatuwezi kuwa na mchunguzi huru, JASIRI, ALIYEBOBEA katika fani hiyo na asiyeshikamana na chama chochote cha kisiasa hapa kwetu Tanzania? Mchunguzi ninayetamani kuwa naye ni kama Muhamed Alli, Mkenya wa kipindi maarufu kama "Jicho Pevu"

Kwa maoni yangu, mchunguzi yeyote aliyeko ndani ya mfumo "system" kama wanaotumika hivi sasa hapa kwetu, kamwe hawezi kutoa taarifa zinazopingana na matakwa ama Interests za mfumo husika. Hakika hatuwezi kujuzwa ukweli wa matukio yanayochukua maisha ya watu wetu kama hatuna mtu jasiri kama huyo Muhamed na timu yake.

Kama kuna mmoja wetu jamani, namtia moyo afanye hivyo, naamini kwa uzoefu wake anaweza kupambana na hila za watawala wetu. Hata akina Mohamed Alli walilazimika kuishi ughaibuni kwa sababu za usalama wa maisha yao. Najua si kazi rahisi, ila MSEMA KWELI NI RAFIKI WA MUNGU!

Naomba mchango wenu wana JF!
 
Back
Top Bottom