Je Hatuwezi kusimama na Kujiamulia Mambo yetu Wenyewe Kama Nchi? ...Silly | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Hatuwezi kusimama na Kujiamulia Mambo yetu Wenyewe Kama Nchi? ...Silly

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ilboru1995, Jun 21, 2012.

 1. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani hawa Watawala na vishoka vyao kama akina Lusinde, Mwigulu, Nape, Komba, Makinda, Lukuvi, Lazaro, Sita, Ndugai, Chenge, Ndullu na wengineo wazungu worshippers! Mnajua kwamba Corporations/Wawekezaji/Wahisani/Wafadhili/Wadhamini of whatever names do strip our natural resources leaving behind trails of environmental devastation. Sadly enough, this is done through our own poor legal frameworks.

  Something is fundamentally wrong with CCM Government...ujinga ujinga mwingi, upuuzi upuuzi mwingi, Ufisadi katika kila pumzi zitokazo ktk matundu yao... madini yanakweda, maliasili yanaondoka, wame temper kwenye sekta ya umeme, wameuza viwanda, mashamba wameua na sasa wameamua kuwapa ardhi yetu hawa waungu untouchable wezi wanaoitwa wawekezaji... silly CCM..

  Sioni future ya Tanzania Jamani... Nini kifanyike wadau? bajeti yenye manufaa kwa mabwana zao itapita tuu yenye misamaha ya kodi kama kawaida huku Taifa litazidi kuangamia...


   
 2. a

  andrews JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 3. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hali tuliyonayo Mkuu ni zaidi ya udhaifu na ujinga... Mbinu zinazotumiwa na mabeberu toka zamani ni pamoja na kuzifanya nchi wanazozinyonya kuwa tegemezi wa kutupwa... wote tunajua roles za IMF na World Bank ktk kuzifanya nchi zinazoendelea kuwategemezi zaidi kiuchumi... magavana wa Central Banki ktk nchi zinazoendelea wamewekwa makusudi ili kufanikisha malengo yao! wote wame/wanafanyakazi na IMF & WB... fanya utafiti utaona mwenye jinsi ambayo hawa jamaa walivyo tuingilia ...
   
 4. regam

  regam JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hatuwezi kwa sababu raisi wetu in dhaifu
   
 5. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu Urais ni taasisi yenye kuendeshwa na mfumo tuliojiwekea wenyewe...Kwanini hakuna accountability? Haiingii akilini kuona kuwa Geita Gold Mine wanatangaza kuwa mwaka huu wameka malego kwa kuzalisha kiasi kikubwa cha dhahabu kinacho zidi makisio yao ya miaka 4 ijayo! sote tunajua kuwa kiasi wanacho disclose ni kidogo sana ukilinganisha uhalisia ... Note kuwa mapato yatokanayo na madini kwa ujumla wake ni 2.7% ya pato la taifa!!! NANI KATULOGA Watanzania?
   
 6. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu sasa neno "dhaifu" sasa limekuwa fasheni basi tumalizie kabisa kwa kulitua kwa wahusika wenyewe - Watanzania! Hakuna Rais wala serikali iwezayo kuingia na kudumu madarakani kama CCM ilivyofanikiwa bila utashi wa wananchi. Kama hatutaondoa virusi vya Ujinga (ignorance); uvivu wa kufikiri na unafiki miongoni mwa sehemu kubwa ya jamii yetu tutaendelea kuwa chakula ya wajanja wa kila aina duniani. Na kuna hatari tutaamka tumechelewa - nchi nzima ikiwa mikononi mwa wageni kupitia uuzwaji wa ardhi (eti ukodishaji wa miaka 99!) na uraia wa nchi mbili!
   
 7. b

  bdo JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Andrews hii jezi inapatikana wapi na kwa bei gani? ninahitaji kama 1,000 tuzigawe hapa mtaani kwetu
   
Loading...