Je, hata hata wanangoja PCCB kuchunguza ndipo washitakiwe?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Baada ya kuona hii habari hadi sasa sijaona tamko la watu kushitakiwa wala kukamatwa naingiwa wasi wasi na juu ya mwenye magogo haya . Je huu si mtego kwamba wanataka kuziba issues za Zitto na Slaa? Mbona kimya mno n ahata waziri kudai magogo kuridi Serikalini? Hakuna sheria ya kuwakamata hawa wafanya biashara wa aina ama ni longo longo za CCM?

Makontena mengine 53 ya magogo yanaswa Dar bandarini
Na Jackson Odoyo

MAKONTENA mengine 53 ya magogo yamekamatwa jana bandarini Dar es Salaam ykwa ajili ya kusafirishwa kwenda nchini China.

Kukamatwa kwa makontena hayo kunafuatia mengine 20 yayokamatwa Jumanne iliyopita usiku eneo la Chang'ombe jijini Dar es Salaam yakiwa njiani kupelekwa bandarini kwaajili ya kusafirishwa kwenda China.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana, Afisa Uhusiano wa Wizara hiyo, Sheiba Lal, alisema makontena hayo mali ya Kampuni ya Micco Import and Export yanakadiriwa kuwa na thamani ya Sh 250 milioni na kwamba kukamatwa kwake ni juhudi za wasamaria wema waliotoa taarifa kisha maafisa wa Wizara wakaweka mitego iliyofanikisha kukamatwa kwao.

"Kukamatwa kwa makontena hayo ni juhudi za wasamaria wema wanaofanya kazi kwa karibu na wizara" ; alisema Lal.

Makontena hayo yalikamatwa siku moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, kusema kwamba serikali imetoa amri ya kufanya upya ukaguzi wa makontena yote yaliyopo bandarini yenye bidhaa za mbao tayari kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Maghembe alisema mbali na ukaguzi huo, serikali itawachukulia hatua kali za kisheria wamiliki wa makampuni yatakayokata miti na kusafirisha magogo nje ya nchi kinyume cha sheria.

Waziri alisema sheria za nchi haziruhusu magogo kusafirishwa kwenda nje ya nchi bali wafanyabiashara hao wanatakiwa kujenga viwanda hapa nchini ili serikali ipate fedha kwa njia ya kodi na wananchi wapate ajira katika viwanda hivyo.

Hata hivyo kauli ya waziri huyo ilitolewa siku moja baada ya serikali kukamata makontena 20 yaliyosheheni magogo ya kiwa njiani kupelekwa bandarini kwa ajiri ya kusafirishwa kwenda China.

Akizungumza katika eneo la tukio Jumanne wiki hii, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Blandina Nyoni, alisema magogo hayo aina ya "Sleeper" ; yalikamatwa baada ya kuweka mtego katika eneo la Chang'ombe, jijini Dar es Salaam baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Nyoni alisema kampuni hiyo ilifanya udanganyifu kwa kusafirisha magogo hayo badala ya mbao kama kibali walichopewa kinavyoonyesha.
 
TAKUKURU wako busy wanakusanya madeni ya TANESCO.
 
Back
Top Bottom