Je, hata baadhi ya wana-CCM wameanza kuona aibu kushangilia matokeo haya?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Kuna baadhi ya wanasiasa kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM) huwa ni wepesi sana kuongelea maswala ya uchaguzi mitandaoni kama vile kupost tweet za kupongeza ushindi wa wagombea wa chama chao huku wengine wakisindikiza tweet hizo na vijembe vya kisiasa kwa wapinzani.

Cha kushangaza ni kuwa nimepitia akaunti za twitter za makada hawa asubuhi hii sijaona popote walipoongelea habari hii ya uchaguzi wa jana wala kutoa pongezi kwa wagombea waliotangazwa washindi na hata kurusha vijembe kwa wapinzani kama ilivyo kawaida yao.

Je, hali hii ni matokeo ya hata wao nafsi zao kuona hawana uhalali wa kushangilia ushindi huu ambao ni wazi si wa haki?

Je, wameanza kutambua hatari iliyopo hata kwa upande wao?

Je, huu si ushahidi kuwa hata kampeni za kuwanadi wagombea wa chama chao wameshiriki kwa shingo upande tu?

Si mawaziri wanaopenda ku-tweet wala wabunge wanaopenda kufanya hivyo ambao mpaka muda huu wameandika chochote akiwemo na bwana slow slow mwenyewe.

Je, ni hivi hivi tu au kuna jambo nyuma ya pazia?

Wacha tuendele ku-observe hali hii tutapata majibu.
 
Wape muda mkuu bado wanakunywa chai huku wakisoma upepo unavumaje uraiani..soon tutegemee vijembe hasa kwa Mwigulu, Nape na Riziwani
 
Hata mimi nimepita kwenye akaunti za wanasiasa wa upinzani kudhania kuwa nitakuta malalamiko kibao juu ya Chaguzi za jana,cha kushangaza hamna kitu,hakuna hata mmoja kati ya wale wapinzani niliyeona ameandika Uchaguzi uligubikwa na wizi na haukua Huru na Haki...
 
Awamu hiii Ccm ni mhimili wa nne wenye nguvu wa nchi.na hiyo mingine mitatu kiasi iko likizo
 
Lil Wayne kwenye wimbo Smell Like Money anakwambia

"It is a shame but niggas are shameless..."
 
Back
Top Bottom