BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,782
Nilikuwa naangalia mechi ya Connecticut leo, bahati mbaya wamefungwa 70 kwa 69. Mtanzania mwenzetu Hashim anaweza kupata kishawishi cha kwenda NBA. Kusema kweli mwaka huu ameimprove sana katika uchezaji wake ukilinganisha na mwaka jana, kwa maoni yangu arudi tena connecticut kwa mwaka mmoja mwingine kabla ya kwenda NBA katika draft ya 2009 ambayo kama kutakuwa na improvement zaidi mwaka unaokuja atakuwa katika top 5 ya draft ya 2009. Kwa wale Watanzania waliomshauri aendelee na masomo badala ya kwenda NBA nawaomba mumshauri tena, anauwezo wa kuja kuwa kama Hakeem Olajuwon wa Houston Rockets ambaye alikuwa ni tishio katika NBA. Wenzangu mnasemaje?