Je, Harmonize alifanya uamuzi sahihi kuuza nyumba zake 3 katika harakati za kujitoa WCB? Wewe ungefanyaje?

Huo mkataba ulikua na thamani ya sh ngapi?
Kama katumilia miaka 4 na kabakiza 6 analipa million 500 basis. Mkataba wake ulikua na thamani zaidi ya Billion 1.
Kwa biashara gani inayofanyika kwenye music industry Tanzania mkataba use na thamani hiyo?
Kwa mkataba huo Harmonize alikua anainhizia kampuni zaidi ya 1.5bilion kwa miaka 10.

KAMBA HII AISEE
Hata mimi nafikilia ivyo mkuu hii ni michezo tu ya mjini apa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Harmonize ametoa hiyo taarifa alipohojiwa na watu kadhaa including MCL, Millard Ayo etc. Nenda Youtube utaona yeye mwenyewe akitoa hio taarifa
Wasanii usiwaamini kwa 100%hata kama wanahojiwa na nani!!...Mimi huwa naamini viunganishi vya maneno tu kama"na".."wa" nk lakini siyo sentensi nzima!
 
Kama show moja anaweza pata 30mil na kauza nyumba zake 3 poa yupo kwenye industry zaidi ya miaka 7 anashindwa vipi kulipa hiyo million 500??
Tatizo usanii kwenye kila kitu...kuongeza 0 tuu ndo jambo mnalojua
Kumbuka hayo mapato yalikuwa yanaenda WCB ye analipwa some %,
 
Ndugu mwandishi, fanya uchunguzi kwanza ndiyo ulete hoja. Ilivyo ni kwamba, mkataba wake wa kufanya hayo malipo sio wa kuilipa hela yote kwa pamoja ila ni wa kulipa hilo deni taratibu kwa kipindi fulani.

Uamuzi wa yeye kuuza au kutokuuza ni wake. Kwani kuzijenga ulimshauri?
 
Kama show moja anaweza pata 30mil na kauza nyumba zake 3 poa yupo kwenye industry zaidi ya miaka 7 anashindwa vipi kulipa hiyo million 500??
Tatizo usanii kwenye kila kitu...kuongeza 0 tuu ndo jambo mnalojua
Kidadari,
Kila kitu huwa ni kwa makubaliano. Uwezo wa kuilipa hiyo hela mara moja anao, ninaamini hivyo, kwa mujibu wa taarifa nilizonazo lakini sheria imeruhusu alipe kwa awamu kadhaa sio mara moja. Jambo ambalo ukiniuliza mimi nitakuambia lipo sahihi kabisa, tena kwa asilimia mia moja. Kwanini? Sijui.
 
Unasema hizo ni kamba kwa sababu inaonesha huifahamu vizuri hii tasnia. Hivi umeshawahi kujiuliza gharama za kutengeneza wimbo mmoja kuanzia audio hadi video?! Tena enzi zile hawa jamaa walikuwa wanategema sana videos production za nje!

Diamond alikuwa akisema video fulani imegharimu takribani 50M, watu walikuwa wanakejeli na kusema anaongeza sifuri mbele bila kufahamu kwamba videos nyingi walikuwa wanatengeneza nje ya nchi na huwa wanaenda huko na crew mzima! Sasa tuachane na hizo 50M, tuseme kila video imetengenezwa kwa ONLY 10M. Je, kwa kuzingatia utitiri wa nyimbo za Harmonize, kwa videos peke yake watakuwa wame-spend shilingi ngapi?!
pesa ya video ishalipwa through yYouTube viewers
 
Hivi kwa nini tukae tunajadili mambo ya mtu binafsi? Baada ya kumjadili huyu, halafu tukurudie wewe kujadili kwa nini ulikula ugali na kisamvu (mfano tu siyo kwamba huo ndio ukweli) siku ya mwaka mpya; nakadhalika. Majadiliano kama haya hayana tija katika kuendeleza nchi.
hahahaaa sawa magufuli kaendeleze nchi
 
Harmonize anapambana ili aweze kuachana kabisa na WCB.

Alitakiwa kulipa shs milioni 500 ili aweze kuwa msanii huria na kufanya kazi zake kama yeye mwenyewe.

Jambo ambalo linamaanisha kwamba kama msanii huria, fedha yote atakayoipata katika kazi zake za sanaa itakuwa ni yake.

Alivyokuwa chini ya WCB alikuwa ni kama mwajiriwa chini ya Diamond na akawa analipwa sio kama mmiliki wa kazi ila kama mwajiriwa wa WCB. Tatizo ni kwamba kutokana na taarifa za MCL, bado hajaweza kuwa msanii huria kwa asilimia zote. Inaonekana bado hajamaliza deni la WCB. Jamaa alishauza nyumba zake pekee ili atoke WCB. Ila sasa deni inaonekana bado halijaisha. Atauza nini tena sasa? Je unavyoona wewe alifanya jambo sahihi kuuza investments zake hizo? Kama ni wewe ungefanyaje?

NB: Muziki na Sanaa ni kazi ngumu. Inahitaji fedha nyingi kufanikiwa. Inaonekana Harmonize sasa atakuwa na madeni makubwa ambayo huwa yanasababisha matatizo ya kifedha. Atapitia wakati mgumu kuwezesha record label yake ya Konde Gang kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Pamoja na yote, tunamuombea kwa Mungu afanikiwe kwa sababu mafanikio ya Mtz mmoja, ni mafanikio yetu wote.
hv kama anauwezo wa kukodi ndege kwa siku moja kwa ajili ya kumpeleka kwao kwenye shoo anashindwa vp kulipa pes
 
Kwani aliposaini mkataba hakuona kwamba utamnyima uhuru? Ni muhimu kufikiri sana kabla ya kufanya maamuzi hasa mambo ya mikataba
wakati ana sign mkataba alikuwa si lolote ni wakati alikua akipigania kula yake kuliko kitu kingine...hakuwa hivi alivyokuwa sasa asingeweza kuleta kiburi...lkn kwa sasa ameshapevuka anaweza akasimama yeye kama yeye..
 
ina maana hizo nyumba 3 zimeshindwa kufikisha m500.....lkn angeulizwa thamani kabla hazijauzwa kila moja angesema inakaribia m800......
 
Back
Top Bottom