Je, Harmonize alifanya uamuzi sahihi kuuza nyumba zake 3 katika harakati za kujitoa WCB? Wewe ungefanyaje?

Harmonize kafanyiwa fair sanaa..

Kuna mijitu humu inaongea kishabiki haijui thamani aliyoachiwa Harmonize ni kubwa kushinda hela anazotoa.

Ni kwamba WCB walikuwa wanamiliki catalog (rights ) za Harmonize, kuanzia nyimbo zake zote, youtube account mpaka hilo jina.

Sasa hebu fikirieni, nyimbo zote alizotoa chini ya WCB katika kipindi cha miaka mitano ijayo zitakuwa zimeangaliwa Youtube mara ngapi ?, zitakuwa zimekuwa streamed spotify , Deezer na kwingineko mara ngapi ?, yaani kwa maana nyingine Harmonize hata asipopiga show yeyote ile au aache muziki leo kuna hela zitaendelea kumiminika kwenye akaunti yake maisha yake yote na hata akifa zitaendelea kuja tuu kwa sababu atakuwa ndiye mmiliki wa catalog yake!!

Sasa kati ya WCB na Harmonize nani kapata faida ?, maana WCB wamepoteza chanzo kikubwa cha mapato ambacho kingeendelea kulipa kwa miaka yote wakati Harmonize anachukua hicho chanzo na kuwa chake yeye mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom