DocJayGroup
JF-Expert Member
- Jan 17, 2020
- 1,654
- 3,319
Harmonize anapambana ili aweze kuachana kabisa na WCB. Alitakiwa kulipa shs milioni 500 ili aweze kuwa msanii huria na kufanya kazi zake kama yeye mwenyewe. Jambo ambalo linamaanisha kwamba kama msanii huria, fedha yote atakayoipata katika kazi zake za sanaa itakuwa ni yake.
Alivyokuwa chini ya WCB alikuwa ni kama mwajiriwa chini ya Diamond na akawa analipwa sio kama mmiliki wa kazi ila kama mwajiriwa wa WCB. Tatizo ni kwamba kutokana na taarifa za MCL, bado hajaweza kuwa msanii huria kwa asilimia zote. Inaonekana bado hajamaliza deni la WCB. Jamaa alishauza nyumba zake pekee ili atoke WCB. Ila sasa deni inaonekana bado halijaisha. Atauza nini tena sasa? Je unavyoona wewe alifanya jambo sahihi kuuza investments zake hizo? Kama ni wewe ungefanyaje?
NB: Muziki na Sanaa ni kazi ngumu. Inahitaji fedha nyingi kufanikiwa. Inaonekana Harmonize sasa atakuwa na madeni makubwa ambayo huwa yanasababisha matatizo ya kifedha. Atapitia wakati mgumu kuwezesha record label yake ya Konde Gang kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Pamoja na yote, tunamuombea kwa Mungu afanikiwe kwa sababu mafanikio ya Mtz mmoja, ni mafanikio yetu wote.