Je, hapa Serikali haijawatapeli walimu? Tafakari hili

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,378
30,829
Kwa mujibu wa mwalimu mmoja aliyepo wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora ambae yupo likizo kwasasa hapa mkoani Dar es Salaam anasema hivi!

Kipindi cha kuelekea uchaguzi walimu waliambiwa na CWT pamoja na maafisa utumishi wajaze haraka sana fomu za Bibi na bwana salary areas claiming forms ili walipwe madai yao haraka.

Ikumbukwe form hizo kuzipata sio rahisi zimewekewa urasimu Fulani hivi wa kishamba kwa mujibu wa mwalimu huyo.

Walimu ilibidi waingie gharama kuzitafuta fomu hizo wakiamini kwamba watalipwa madai yao kabla ya uchaguzi.

Hamaaaaadi yule mwalimu alipopeleka barua yake ya likizo akaulizia areas zao zimefikia wapi? Akaonyeshwa luuuundo la ile mifomu ikiwa Imejaa vumbi hiyo ndio Asante ya CCM kwa walimu.

Baada ya kuwatumia kama pampasi kuiba kura Sasa hamna thamani teeena.

Five mooooo ooooo Kama mlio wa ng"ombe.
 
Japokuwa ni sekta muhimu ya kuelimisha kizazi. Walimu wamebaki kuwa kundi lisiloweza kujifunza . Na limekuwa likirudia makosa all over again.. year after years.

Wanahitaji ukombozi wa fikra otherwise watalalamika for the rest of their lives.
 
Na ndio maana wanadharauliwa Sana Mimi nimewafukuza walimu wote waliopanga kwenye nyumba yangu kwa kisingizio Cha ukarabati.

Aah, that's not good at all...

Nina hakika umewaonea tu baadhi yao. Na kama bado walikuwa wanaishi nyumba ya kupanga, basi hao ni walimu vijana walioanza kazi five years ago...

Walimu wakongwe wenye umri wa miaka zaidi ya saba kazini na kuendelea na wenye akili na maarifa wana makazi (nyumba) zao binafsi...

By the way, ni walimu wachache sana wanaoisadiaga CCM...

Trust me, majority wako against na hawaupendi kabisa utawala huu wa Magufuli na CCM yake...

Fanya utaratibu uwaombe radhi walimu hao na ikibidi bring them back in the house. Ni vijana wadogo hao. Ni makosa kuwa - punish kwa mawazo ya kufikirika...
 
Shida kada ya ualimu imedumazwa,imedharaulika na inalipwa kajimshahara kadooogo tena skuizi hawapandishiwi hata madaraja ipasavyo labda wale walimu wazee kazini ndiyo mishahara walau inakutana!!
Nasemaga huyu waziri asiyestaafu mh. Mkuchika mbona anaonekana kama anabusara? Kama hasikilizwi kuhusu maslahi ya walimu kwanini asikae pembeni anachuma dhambi uzeeni? Au yeye anashiba hajali mateso walimu wanapitia??
Wakipewa kakazi kakuingiza hata elfu kumi wanakimbilia mpaka kudondoshana... Poleni walimu kwa mateso mnayopitia
 
Wewe huja
Walimu ni miongoni mwa makundi yaliyosaidia kuiba kura za ccm..sina ham nao kabisa
Hivi wewe hukufundishwa na mwalimu fulani ulipokuwa shule kusoma na kuandika?,hii ndiyo jaza yako kwa mwalimu wko?
Haya na iwe hivyo.
Bali mwaka huu sisi hatukuhusishwa kabisaa kwenye mchakato wa kura ,kama ilivyokuwa chaguzi za zamani.
sasa linganisha chaguzi zilizosimamiwa na sisi miaka ya nyuma na huu uliosimamiwa na makada wa CCM mwak huu.

Musituonee jameni,sisi ni watu na tunaumwa sana kwa yanayojiri nchini kwetu, hatuna nguvu tuu
 
Mkuu nami pia ni mwalimu, tena mwalim mwenye uzoefu wa kutosha na ni graduate ....ila nlichosema hapo juu nakifaham

Wako walimu kadhaa hapa waliosimamia uchaguzi uliopita, wanasema wazi uchafu walioufanya aidha kwa sababu ya ukada wao au kupokea maelkezo toka kwa wakurugenzi...

Kwa hivo ni kweli walimu wenzetu walihusika kwa namna moja au nyingine kwa kuiba kura za ccm.

Japo hiyo haikusaidia chochote kwa kutangaza wagombea wa cc kuwa washindi.....
 
Nakuelewa, lakini kimsingi kesi ya wachache haiwezi kuchukuliwa kwa wote,.
ukweli ni kwamba hao hawakushiriki kama waalimu, bali walishiriki kama makada wa CCM.

Wame rise Issue ya ualimu wao baada ya kuona maslahi mapana ya walimu yametapeliwa.
Hata hivyo ukuwauliza ualimu na ukada bora nini? watakuambia ukada ni bora.
 
Kwa mujibu wa mwalimu mmoja aliyepo wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora ambae yupo likizo kwasasa hapa mkoani Dar es Salaam anasema hivi!

Kipindi cha kuelekea uchaguzi walimu waliambiwa na CWT pamoja na maafisa utumishi wajaze haraka sana fomu za Bibi na bwana salary areas claiming forms ili walipwe madai yao haraka.

Ikumbukwe form hizo kuzipata sio rahisi zimewekewa urasimu Fulani hivi wa kishamba kwa mujibu wa mwalimu huyo.

Walimu ilibidi waingie gharama kuzitafuta fomu hizo wakiamini kwamba watalipwa madai yao kabla ya uchaguzi.

Hamaaaaadi yule mwalimu alipopeleka barua yake ya likizo akaulizia areas zao zimefikia wapi? Akaonyeshwa luuuundo la ile mifomu ikiwa Imejaa vumbi hiyo ndio Asante ya CCM kwa walimu.

Baada ya kuwatumia kama pampasi kuiba kura Sasa hamna thamani teeena.

Five mooooo ooooo Kama mlio wa ng"ombe.
Mialimu ya Tanzania haina akili tena wacha ikomeshwe!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom