Je Hamadi Rashid atahamia wapi baada ya kuondoka/kufukuzwa CUF?

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
WANAJF;
Hali inaonyesha si shwari ndani ya CUF na hasa kwabunge wa Wawi Mh. Hamad Rashid, na hivyo kuna uwezekano mkubwa tu wa yeye kufukuzwa au kuondoka yeye mwenyewe ndani ya CUF na kwenda kwenye Chama kingine au kuanzisha Chama chake. Hali hii inajidhihirisha wazi pale jana baada ya kukataa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Chama chake cha CUF kwa madai kwamba hakiko kwa kuzingatia Katiba ya CUF. Lkn pia alpowaita Waandishi wa Habari alitoa shutuma nzito sana kwa Viongozi wake wa juu wa Chama. Kwa hali ilivyo sasa, naamini kabisa kwamba siku za Hamad Rashid ndani ya CUF zinahesabika, labda atakapoamua kutumia nguvu ya Mahakama ili aendelee na nafasi yake Ubunge na Uanachama wa CUF. Na hata kama atafanikiwa ktk hili, lkn atakuwa hana umaarufu tena ndani ya CUF, kwani tayari ameonekana msaliti ndani ya Chama.

Yawezekana madai ya Hamad Rashid ni ya msingi, lnk ni kwanini ameshindwa kwenda kutoa maelezo kwenye kikao cha Chama kwani mara nyingi amekuwa akitoa shutuma zake nje ya vikao? akilalamika kwamba hajapewa nafasi ya kusikilizwa, sasa yeye anataka asikilizwe wapi? Mimi naamini njia anayotumia Hamad Rashid haijengi na badala yake inabomoa mustakabali wa CUF. Kwani taswira ambayo Hamad Rashid ameonyesha si ya kiungwana kabisa dhidi ya Chama chake na Viongozi wake, kwani badala ya kwenda kwenye Kikao yeye anawaita waandishi wa Habari na kuendelea kutoa shutuma dhidi ya Viongozi wake. Hizo documents anazosema kwamba anazo za kutaka kumfukuzisha kwenye Chama, si angezitumia mbele ya Kamati na kuonyesha kwamba yeye yuko sahihi na ni kweli anaonewa.

Kwa ninavyomfahamu Mh. Hamad Rashid toka mwaka 2000 alipokuwa Bungeni, ni kweli alikuwa ni mtu makini sana katika kujenga hoja hasa kipindi alipokuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Tatizo lilikuja kuanza mwaka 2010 hasa baada ya yeye kukosa nafasi ya kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Hapo ndipo Watanzania tulipopata nafasi zaidi ya kumfahamu Hamad Rashid kama mtu ambaye yuko tayari hata kukidhoofu kambi ya Upinzani kwasababu tu yeye hajapata nafasi ile ya kuwa Kiongozi. Ni huyu huyu Hamad Rashid ndiye aliyeweza kuwashawishi Wabunge wengine wa Upinzani ili wasiungane na CHADEMA na kuanzisha kambi nyingine ndogo (Minority) ya Upinzani. Na Hamad Rashid alijua fika kwamba kwa kufanya hivyo alisaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza sauti ya pamoja ya Vyama vya Upinzani Bungeni. Na madhara ya hiki alichokifanya kimeonekana hasa katika mjadala wa suala la KATIBA MPYA kwa ajili ya Watanzania wote, kwani hata yeye Hamad Rashid alisimama kidete kuwashutumu na kuwabeza Wabunge wa CHADEMA waloamua kupuuzia mjadala huo. Katika hili la Katiba ilituumiza hata sisi Wana-CCM ambao ktk hili tungependa muangalie maslahi ya nchi yetu ya Tanzania na si maslahi ya CCM, kwani vyama vitapita tu lkn nchi itaendelea kuwepo. Mimi naamini kabisa kwa Wabunge kama Mh. Kafulila, Felix na hata Machali nao kwasasa wameona ni kujua kwamba kumbe Hamad aliwashawishi tu kwasababu ya Kukosa nafasi ile ya Uongozi Bungeni.

Sasa huyu Hamad, baada ya kuona kwamba kambi ndogo aliyofanikiwa kuiunda Bungeni na kupunguza nguvu ya Upinzania haina maslahi kwake, ameanza tena chokochoko ndani ya Chama chake cha CUF, kwamba anataka kugombea Ukatibu Mkuu wa Chama. Tatizo si kuonyesha nia ya kutaka kugombea, tatizo ninaloliona hapa ni kwamba njia anazotumia si halali kwani si vikao halali vya Chama. Hamad amekuwa akitumia njia ya Waandishi wa Habari na hata kufanya Mikutano isiyo na go ahead ya Ofisi kuu ya CUF ktk kulifanikisha hili. Ni njia hizo ambazo ziko nje ya utaratibu ndiyo maana CUF nacho kinamlalamikia kwamba hafuati utaratibu ili kuboresha dhana ile ya majadiliano ndani ya vikao husika.

My Take: Kwasababu Hamad Rashid anasumbuliwa sana suala la UONGOZI, ningependa kumshauri AANZISHE CHAMA CHAKE ili awe na nafasi hiyo ya kuwa Kiongozi kama anavyotaka iwe kwake siku zote. Pia niwashauri Vyama vingine hasa CHADEMA ambacho kimeonyesha mwanga kwamba; MKIJIDANGANYA mkampokea Hamad Rashid, basi mjue ndiyo mwanzo wa migogoro na mwisho wake Chama hakitakuwa na Mwanzo mzuri. Kwa CHADEMA, na vyama vingine, Hamad Rashid ni hatari sana kwenu hata akiwa Mwanachama wa kawaida tu. Labda arudi CCM, kwani huku kwetu tuna njia nyingi sana za kuweza kuwatuliza.
Nwasilisha.
 
Alishasema kuwa ikitokea akafukuzwa au kujitoa CUF ataanzisha chama kipya KIKUBWA cha siasa...!
 
Kwa kawaida wanaohama CUF huenda kujiunga kanisani...................................

Refer, Akwilombe, Rwakatare. Prof. Abdala Safari nk..
 
Kwa kweli hamad rashid kuna jengine nyuma ya pazia ambalo amelificha na sio ukatibu mkuu ndani ya cuf.


Maana kaanza na kutunga kitabu cha ''yaliojiri' na kwa mwendo unakwenda tujipange kusikiamengi ambayo huenda yakatuacha midomo wazi


siasa kweli si hasa baadhi ya wakati
 
Unamlaumu Hamad Rashid wakati alikuwa akitekeleza agenda za chama CUF... kwa nini unamtazama yeye kama mtu alokuwa Chadema au chama kingine kwani kila alichokubalia maa kupinga bungeni ndivyo alivyoagizwa na chama chake kusimamia..
 
anaweza kwenda cdm, ila ni baada ya mazungumzo mazito. Atakabidhiwa zanzibar na atateuliwa kuwa mgombea mwenza. Siasa ni kitu ingine kabisa
 
hamad ni dili kwa chadema ni kumvumilia kumuweka sawa kumbuka cdm haina watu zmz,bpra hamad kuwa mgombea mwenza kuliko yule jamaa aliyeingia mtini kwenye kampeni.hakuna adui wala rafiki wa kudumu kweye siasa
 
Back
Top Bottom