Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Huyu ni Mheshimiwa Halima James Mdee, Mbunge wa Jimbo la Kawe Jijini Dar es Salaam. Kwenye hii picha anaonekana akimvuta shati Askari wa Bunge mpaka kuichana sare ya Askari huyo. Mdee alikuwa anawazuia Askari hao wasimtoe ukumbini Mbunge wa Kibamba, Mheshimiwa John Mnyika aliyefanya kosa la kudharau kiti cha Spika na hivyo Spika Job Ndugai kuamuru atolewe nje.
Kwa kuwakumbusha tu ni kwamba, Bunge kwa umoja wao walimsamehe Halima Mdee kutokana na kosa la kumtukana Spika Ndugai kwa masharti kuwa hatafanya tena kosa. Na endapo atafanya tena kosa, ataadhibiwa bila hata ya kuitishwa Kikao cha Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge.
Kwa ushahidi huu ni wazi kuwa Halima Mdee anakabiliwa na adhabu kali sambamba na mwenzake Esther Bulaya ambaye naye alisamehewa kwa masharti.
Kwa mtazamo wako, je unadhani Halima Mdee anastahili tena msamaha wa Bunge? Au safari hii apewe adhabu kali ili ajutie makosa yake?