Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Kwanza jibu hili

WEWE KWANINI ULIKATWA UCHAGUZI WA NDANI?
Mimi sikukatwa uchaguzi wa ndani, anayekatwa ni yule aliyeshinda kura za maoni, halafu vikao vya uteuzi vikalikata jina lake na kumchukua mshindi wa pili au watatu.

Mimi ni wajumbe walifanya yao, kura hazikutosha.
P
 
Mimi sikukatwa uchaguzi wa ndani, anayekatwa ni yule aliyeshinda kura za maoni, halafu vikao vya uteuzi vikalikata jina lake na kumchukua mshindi wa pili au watatu.

Mimi kura hazikutosha.
P
Wewe si kwamba tu hazikutosha walikuona haufai kabisa, mimi nakufahamu wewe tokea mwanza paschal si mtu sahihi kabisa. Kama unashabikia mtu kama gwajima aisee paschal nazidi kukuondolea nyota kabisa.
 
Paskali, ukiona hadi wanyama hayawani (mbuzi, sijui kama mbuzi kweli ) wanabandua picha ya mgombea wako, ujue huo ni ujumbe tosha. Gwajima bado sana kuwa mbunge. Gwajima amechanganya sana madesa, muacheni kwanza ayaweke sawa then mara nyingine ateuliwe agombee kama atakuwa ameshatubu kumkufuru Mungu.
 
Wewe si kwamba tu hazikutosha walikuona haufai kabisa, mimi nakufahamu wewe tokea mwanza paschal si mtu sahihi kabisa. Kama unashabikia mtu kama gwajima aisee paschal nazidi kukuondolea nyota kabisa.
Anamuunga mkono Gwajima ili aonekane alivunja kambi ya kampeni na kurejesha umoja utakaisaidia ushindi ili baadaye ahurumiwe apewe teuzi.
 
Wewe si kwamba tu hazikutosha walikuona haufai kabisa, mimi nakufahamu wewe tokea mwanza paschal si mtu sahihi kabisa. Kama unashabikia mtu kama gwajima aisee paschal nazidi kukuondolea nyota kabisa.
It's true wajumbe wana uhuru kamili wa mawazo yao, hivyo they are right kumuona mtu yoyote hafai, ila kuna uwezekano baadhi ya waliopitishwa, mimi nina afadhali!.

Unaweza kuiangalia self assessment yangu kama Mbunge, nilitaka kwenda Bungeni kufanya nini?
Je, wajua kuna watu wazuri, waadilifu wenye uwezo, wanaotaka kuingia Bungeni kulisaidia Taifa, Bunge na kumsaidia JPM kwa dhati, lakini kwa vile...
P
 
Ukiacha ile kauli yake ya udini, naona Gwaji upepo kdg unaanza kumuendea vzr hii style ya kuzunguka mtaa kwa mtaa ,nyumba kwa nyumba inamuweka karibu na watu
 
Mwanasheria na mwanahabari msomi, kazi ya mbunge ni kuwakilisha wanajimbo wake Bungeni, Kazi ambayo Mh Mdee ameifanya vizuri. Kazi ya kujenga miundombinu jimboni ni ya serikali inayokusanya kodi. Hata Mdee akitumia mshahara wake kujenga barabara ya lami, hautoshi hata kumaliza km 1. It is sad that hata wasomi wetu hamwelewi such a basic fact. Expectations za watu kwa mbunge kujenga miundombinu ni za kipumbavu na zinafanya maisha ya wabunge kujaa stress.
Wanabodi,

Mimi ni mkazi wa Kawe, kwa vile sasa tuko kwenye kampeni za uchaguzi, ili tumtendee haki Mbunge wetu aliyemaliza muda wake, Mhe. Halima Mdee, ambaye, baada ya kuwa Mbunge wa Kawe kwa vipindi viwili mfululizo, na sasa anaomba tena tumchague, hivyo nauliza kama kuna mtu yoyote anaweza kutueleza humu, hata jambo moja tuu, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, amelifanyia nini jimbo la Kawe katika kipindi chake chote cha miaka 10?, ili tumfanyie assessment kama anastahili jee anastahili kuongezewa miaka mitano mingine, or she did nothing hivyo anastahili apumzishwe?

Declaration of Interest
Japo mimi Paskali Mayalla kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, lakini bandiko hili sio la ukada au propaganda za kampeni za uchaguzi, bali ni bandiko hojaji ya halali na swali la ukweli la mwana Kawe, kuuliza Mhe. Halima Mdee ameifanyia nini Kawe in the past 10 years kustahili kuendelea?

Rais John Kennedy wa Marekani aliwahi kusema, " usijiulize Marekani imekufanyia nini, bali ujiulize, wewe utaifanyia nini Marekani". Mhe. Halima Mdee ndie Mbunge wetu Kawe kwa kipindi cha miaka 10, naomba kuuliza kwa anayejua, Jee Halima Mdee ameifanyia nini Kawe?.

Najua kuna watu watasema kazi ya kuleta maendeleo ni kazi ya serikali, kazi ya Mbunge ni kuisimamia serikali, tumekuwa tukishuhudia wabunge wa majimbo mengine wakipigamia majimbo yao Bungeni, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, aliwahi kupigania nini cha maendeleo ya Kawe?. Kama kuna anayejua humu, atuambie hata kitu kimoja tuu cha Kawe ambacho Halima Mdee alikipigania?.

Kuna zile fedha za Mfuko wa Jimbo. Jee kuna mwana Kawe yoyote, aliwahi kumshuhudia Mbunge wetu Mhe Halima Mdee akija eneo lolote la Kawe na kuchangia shughuli zozote za maendeleo kupitia fedha za mfuko wa Jimbo?.

By the way: Leo nilikuwa mahali nikamsikia Askofu Gwajima, kumbe huyu Askofu ni mdau mkubwa wa maendeleo ya watu wa Kawe kwa kipindi kirefu na ameisha fanya mambo makubwa kwa wana Kawe kama Mwananchi tuu wa kawaida bila hata kujua kuwa kuna siku atakuja kugombea ubunge wa Kawe.

Kumbe Askofu Gwajima baada ya kuhamia Kunduchi Salasala, alikuta kuna tatizo la maji. Na kufuatia eneo la Kunduchi ni eneo la pembezoni mwa bahari, ukichimba visima vifupi, utapata maji ya chumvi, Hivyo Askofu Gwajima kwanza alichimba visima virefu 12 vya mita 300 kwenda chini ili kupata maji safi na salama kwa ajili ya wana Kawe!. Miongoni mwa wafaidika wa visima hivyo virefu, kwenye misikiti 7 ya Salasala hivyo kuwapatia maji Waislamu, maji ya kutawadha kabla ya kuswali.

Kisha akayatafuta maji ya Dawasco, yanapita mbali, akaomba kibali Dawasco, akanunua manomba kama ya Dawaco ya kusambaza maji, akayatandika kuwatumia mafundi wa Dawasco, anunua pump ya mamilioni kutoka Ujerumani, akanunua mita za maji kama za Dawasco na kusambaza maji kwa kaya 250 za majirani wake wanaomzunguka, sasa wanapata maji safi na salama!.

Askofu Gwajima tayari ameisha saidia magari 7 ya ambulance za wagonjwa kwa hospitali mbalimbali, na kuahidi atazipatia magari ya wagonjwa hospitali za Kawe na Kinondoni.

Gwajima amesema, kazi ya kuwaletea maendeleo Watanzania sio kazi ya serikali pekee, ni kazi ya wananchi kwa kushirikiana na serikali, hivyo hapo alipo, tayari ameagiza tinga tinga la kuchonga barabara na malori mawili ya tipper, ambapo barabara zote za Kawe na Kinondoni zitachongwa, vijana wa Kawe watapatiwa ajira za kuchimba mitaro ya maji, hivyo kama ni serikali, itabaki kazi ya kuziwekea tuu lami!.

Mwana Kawe yoyote akiyasikia haya Askofu Gwajima aliyoyafanya Kawe, kabla hata hajawa Mbunge, ukilinganisha na alichofanya Mhe. Halima Mdee kipindi chake chote cha miaka yake 10!, ukiambiwa umchague mmoja kati ya hawa wawili, utamchagua nani?.

Utakubaliana na mimi kuuliza, Jee is it, it's high time, tumshukuru Mhe Halima Mdee kwa utumishi wake wa miaka 10 Kawe?, na tumuage kwa upendo, heshima na taadhima kwa kumwambia, Bye Bye Mhe. Halima Mdee Kawe, asante sana kwa utumishi wako wa miaka 10 Kawe?, na Jee sasa tumkaribishe Askofu Dr. Josephat Gwajima kwa kumwambia, "karibu, Kawe Askofu Gwajima ili kuikamilisha kazi nzuri ulioshaanza kuitenda kabla hata hujawa Mbunge?.

Kama kuna mtu yoyote ana video clip yoyote ya Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee akishiriki shughuli yoyote ya maendeleo Kawe, naomba aielete ili angalau tumuone!
Shuhudia mwana Kawe huyu anavyojituma kwenye kuleta maendeleo

View attachment 1558915

Nauliza tuu!.

Paskali
 
It's true wajumbe wana uhuru kamili wa mawazo yao, hivyo they are right kumuona mtu yoyote hafai, ila kuna uwezekano baadhi ya waliopitishwa, mimi nina afadhali!.

Unaweza kuiangalia self assessment yangu kama Mbunge, nilitaka kwenda Bungeni kufanya nini?
Je, wajua kuna watu wazuri, waadilifu wenye uwezo, wanaotaka kuingia Bungeni kulisaidia Taifa, Bunge na kumsaidia JPM kwa dhati, lakini kwa vile...
P
So unasema gwajima hakufaa kabisa kuteuliwa kuwa mgombea wa kawe???
 
Naona mlioshindwa kura za maoni mnatekeleza agizo la Mwenyekiti wenu kuwapigia debe waliopita!Hapa unajiwekea kafursa ili ukumbukwe kwenye teuzi kwa kutii maagizo ya mwenyekiti!Huwezi kutenganisha ukada wako na mawazo yako,kwa wanaJF utakuwa mnywa maji ya kijani tu!

Kujijengea heshima fulani na kuaminika inachukua muda mrefu,ila kuvivunja vitu hivyo ni ndani ya sekunde moja tu!

Ulishapoteza hilo na huenda mpaka unaingia kaburini,level ya heshima uliyokuwa nayo JF isirudi tena!

Ni bora ukubaliane na hali na uwe kijani kweli kweli,,kuwa kama polepole tu!
straight talk
 
Paskali nisiwe mnafiki siwezi mchagua Gwajima kwakuwa alishasema anataka kuigeuza misikiti kuwa Sunday schools, nikiwa kama muislam nawaza huyu hakuwa na madaraka aliongea vile je nikimkabidhi madaraka itakuwaje? Mimi ni muislam na najivunia kuwa muislam
Naona wewe unajibu swali ambalo halijaulizwa; ingekuwa mtihani ungepata sifuri
Mtoa mada ameuliza atajiwe mambo aliyo yafanya Halima Mdee kwa miaka 10; wewe unaleta swali tofauti kabisa na kulitoa jibu? Jifunzeni basi kujibu maswali
 
Akagombee Uaskofu Mkuu wa makanisa ya TAG lakini sio Ubunge.
Hatutaki udini na ukabila hapa Tanzania .

Kuna baadhi ya watu wa dini nyingine wanakwazwa na huyu ASKOFU lakini wanamvumilia wakijua kuwa anahubiri dini yake kumbe anawaza kuingia serikalini ili atimize azma yake ya kugeuza misikiti kua kumbi zake za Kuwashambulia watu kama alivyomshambulia Kadinali Pengo.

Kama anafaa sana kuwa Mbunge kutokana sifa alizonazo kwa awamu hii basi Kuna nafasi kumi za Uteuzi wampe moja.

Na tumeharibiwa sana nchi yetu. Tunadanganywa maendeleo hayana Chama lakini mtu akijaribu kuhamasisha maendeleo basi ni lazima ajiingize kwenye siasa za CCM au ajipendekeze kwa watawala.
Sadaka anazokusanya kutoka kwa maskini na misaada toka kwa mabeberu anazitumia kwenye siasa badala ya kutangaza injili na kuwasaidia wasiojiweza.

Wanakawe wa dini zote tumtie adabu huyu mdini mwenye imani Kali na muasi kwa kumnyima kura .

Siasa ni fani awaachie wenyewe . Vinginevyo asimame kwenye kweli ya neno la Mungu na aonyeshe kukerwa na siasa za kibaguzi za CCM na dhulma ambazo anazitegemea zimpe kura za wizi.
Awe tu tayari kukataa kura za wizi ili asianguke kwenye mtego wa shetani.

Halima Mdee aliwawakilisha watu wake Jimboni ipasavyo ndio maana alikua anafukuzwa Bungeni huku bunge likiwa gizani ili tusione dhulma walizokuwa wanafanyiwa wapinzani hasa Halima na Sugu.

CCM isiangalie Kawe tu yapo Majimbo mengi sana itapoteza kutokana na Dhoruba ya ghafla iliyowafikia baada ya kurejea TL.
Mwaka huu ni Mwendo wa sala na Albadir mtu atakayeharibu uchaguzi lazima awe kichaa au ajiandae tu kivingine mana Albadiri haitamuacha mtu.
Wamemdhihaki Mungu vya kutosha.
Watu wanasema tumweke Mungu mbele halafu wanafuta formu za watu ili zionekane zimekosewa.
Watu walioapa kutenda haki wanafanya uhuni na dhulma bila hofu.
Watu wanajipendekeza kwa wanadamu kuliko kumtii Mungu.

Hivi Gwajima anaweza kumlaumu JK wakati Makanisa yote ya watu Binafsi yalistawi kipindi cha JK.
Ukata ndio umewapelekea kwenda kuwasujudia watawala na kumdhihaki Mungu.
Kama walimdhihaki JK wakati aliwapa fursa wengine wakafungua mpaka Mabenki ya Hayo makanisa yao leo hii wanakimbilia siasa ili wajiweke kwenye nafasi ya kuonekena mbele za watu.

Ni Lini Sadaka zinazotolewa kwa ajili ya Misikiti ikatangazwa?

Hivi mtu kama Bakhressa akitangaza kuwa ametoa misaada kwenye misikiti si itabidi agombee Urais kabisa ??
Yani tuvisima tuchache alivyochimba ndio anajiona amekua ni mdogo wake mtume Muhammad ,mtume wa Mwenyezi Mungu.

Waislam Msimchague Gwajima kwa Kusumangwa na Visima mbele ya watu.
Sadaka huwa ni siri kama alivyoelekeza mwenyezi Mungu.

Alitoa misaada kama sehemu ya sadaka anazopokea . Sasa asitumie sadaka hizo kama wakoloni kuwa fimbo ya kuwatawala watu na kuwafanya watumwa wake. Hakuna mtu aliyemuomba Bali aliamua mwenyewe.
Na sisi atuache tuamue wenyewe kumpa kura au kutompa .Asitupangie.

Majimbo ya CCM hakuna mtu anayeruhusiwa kutoa rushwa kama misaada wakati wa kujipanga ili achaguliwe lakini kwa wapinzani ni Ruksa kama alivyofanya Gwajima na Tulia Aksoni kwa miaka mitano.
Na wote wataangukia Pua. Huyu akienda Bungeni atarejesha sheria ya Rushwa kama ilivyokua awamu ya tatu iliyotuletea Rushwa ya Takrima bila aibu.

Haki huinua Taifa .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom