Je hali ya Huduma za Jamii Tanzania sasa Ni Bora?

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Kila Nikisoma Magazeti Na Mitandao, Naona habari za Kufukuzwa Huyu, Rais Kamkoromea jamaa huyo. Waziri Kawachimbia Mkwara hawa. Mkuu wa Mkoa kamwambia mtu, asije na suti na tai akitegemea kufanyiwa kazi zake?

Na wakati Mwinge yaani hata Makonda naye anawekwa Kurasa za mbele za Magazeti akifanya Drama zake.

Ila Nisichoweza Kuona ni, Vipi Muhimbili Wagojwa sasa wanapata dawa na matibabu kwa wakati?
Vipi waalimu wanalipwa kwa wakati? Je wanapewa angalau chaki? au wanaandikia Kisena (Pozzolana) Je watoto wanamadarasa ya Kutosha au bado wanasoma chini ya Miti, Je wana madawati? Je wanavitabu?

Je Mwananchi anaishi Kwa Raha nchini mwake au bado kuna Tabia ya Polisi Kupiga/Kunyanyasa Raia? Je sheria Kandamizi zinaondolewa au Ndio Kwanza Zinaongezwa nyingine za Upuuzi?
Je Ubeberu Zanzibar umeisha, au wananchi wa Zanzibar bado wanishi katika hali ya hatari katika Ardhi yao waliopewa na Mungu?

Haya Ndio ya Msingi, Sio Maigizo, hata ya Makonda ndio Mnatuandikia Kila Ukicha! We need Real News not these vexing dramas.
 
Acha tupumue kwanza mkuu. Bado tunasoma mchezo tujue wananchi wanataka nini. Shaka ondoa Serikali ya Viwanda itatimiliza yote na utafurahi tuu.
 
Back
Top Bottom