Je, Haki za Binadamu ni Exceptional?

alumn

JF-Expert Member
Jul 15, 2018
2,366
3,109
Nimesoma tukio lililotrend mitandaoni wiki hii la Msanii na Mjasiriamali Maarufu Tanzania kupigwa na Mumewe.

Binafsi ninakemea vitendo kama hivi kwani havina taswira njema kiutu, kijamii na hata kihisia ninakemea na kweli ninapingana na aina yeyote ya unyanyasaji.

Kupitia tukio hilo nimeona baadhi ya watu wakitoa mitazamo yao mbalimbali na ama kwa hakika wamekilaani kitendo hicho sana na wakafika mbali zaidi kwa kumtupia lawama nyingi Bwana Uchebe na baadhi kwenda mbali zaidi kwa kuwatukana Wanaume pia.

Ndugu zangu kupitia tukio hili Nina mengi ya kujiuliza juu ya hili neno Haki za Binadamu. Mlengo hasa wa hizi haki je ni Mwanamke pekee? Ndiye mwenye haki. Je iweje tukio la kupigwa huyu Dada kama ni kweli lakini lichukuliwe kwa uzito kiasi hiki. Kuna wanaume wangapi wanaonyanyaswa na kuteswa na wake zao ambao hawajitokezi na kueleza masaibu yao na hata wakijitokeza uzito wao umekua si sawa na Hawa dada zetu wanavyopewa uzito? Au sababu yeye ni msanii? Je maneno kama ya Baba Levo kwa mkewe Uchebe kua Katika safari yao kila wakipiga tuta Titi linatoka nje anarudisha yalikua ni maneno mazuri kweli kwa Mmewe kuyasikia. Assume wewe Mkeo mtu amuongelee vile unajisikiaje? Ila hilo likachukuliwa kawaida tu.

Watu wanamtuhumu Uchebe kwa sababu ya hilo tukio je? Wanajua yaliyo nyuma ya Pazia ya watu hao wawili yanayowahusu? Kama haitoshi watu wanaenda mbali na kusema Mwanamke hapigwi kumbe mwenye haki ya kupigwa ni nani Ndugu zangu nauliza tafadhali nipate majibu.

Niseme wazi Utandawazi umeleta mambo mengi kwenye jamii zetu. Watu hawa mda wanatongozana sisi hatukuepo na pia sote hatujui heshima na wajibu wa Mke na Mme ndani ya familia hii ulikuaje, kuna mda tunachuma dhambi kwa kujihushisha na kuhukumu mambo yasiyotuhusu. Ni vyema kuacha Mamlaka husika kupatia ufumbuzi kwa mambo kama Haya kuliko kua werevu wa kuhukumu na kilaumu bila kujiridhisha na kua na hakika.

Kupitia tukio hili na michango mbalimbali ya Wadau kama Taifa tuna safari ndefu sana ya kua na wababa imara katika familia na likini pia Wamama shupavu wenye kusimama na kuratibu maswala ya kifamilia.

Unyanyasaji Aina yeyote ule kwa mtu yeyote ule haukubaliki tuishi katika misingi ya Upendo, Heshima na Kiasi kusiwepo na hali ya Gender au Race flani yenye priority zaidi ya nyingine kua huyu akifanyiwa hivi ni tukio kubwa sana ila mwingine akifanyiwa vile inachukuliwa kawaida na kuambiwa maneno rahisi rahisi kama kaza moyo na Mezea Moyoni. HAPANA.

Yamkini hata humu kuna wakakana Wababa wanapigwa tu vizuri na wake zao au wapenzi wao ila ilachukuliwa kawaida ila kwa Mdada au Mke ikitokea inakua ni Habari Kubwa. Sote tuna wajibu wa kuishi kwa Misingi na Taratibu bila kuumizana.

Nawakilisha Mtazamo wangu.
 
Alisema hataki upumbavu wakati anamtia vibao Nuh sasa kakutana na Uchebe hataki ujinga kabsaaa🥱🥱🥱
Lakini kipigo kama kile hakifai bora utemane nae tu.
 
Mimi wanawake zangu nawaambiaga kabisa hakuna wakunizuia kukunyoosha tabia ukileta upumbavu kuwa makini!

Hautaki kunisikiliza nenda kwa hao ustwawi/watetezi ukakae nao.

Kusikia kwa kenge mpaka atoke damu masikioni.
 
Back
Top Bottom