Je, haki yangu nitaipataje kutoka kampuni hizi za simu?

Mtafiti77

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,841
2,270
Mimi ni mteja wa kampuni mbili za simu; tigo na vodacom. Cha ajabu mitandao hii imekuwa na tabia ya kuniibia pesa kwa hila. Walianza vodacom wakishirikiana na kampuni ya pushmobile. Kupitia huduma waliyoiita burdani wamekuwa wakinitumia msg za ajabu pengine wakidhani kwangu ni burdan kumbe hapana. Kila wakinitumia hukata kiasi cha sh. 150/=. Kwa sasa hao wazee wa burdan wamestop wamezua huduma iitwayo ''mwananchi'', sijui kama inaamaanisha gazeti au la! Nao pia wamekuwa wakinitumia taarifa kwenye line ya tigo na voda. Nao pia hukata 150/= kwa meseji.

Napenda kuwataarifu wanajamii, nipo timamu wala si mlevi; mimi sijawahi kujiunga kwa namna yoyote ile na huduma hizi.Labda mtu anisaidie huenda kuna mtego makampuni haya yameweka labda wakati napokea simu zangu pengine ndiyo niwe nimejiunga au vinginginevyo! Nikijaribu kuwapigia huduma kwa wateja sipati msaada hasa vodacom, tigo huwa nawapigia huduma kwa wateja bila mafanikio. Simu zangu hazishikwi na mtu yeyote! Kwakweli mpaka ntakaposhawishika kwa maelezo thabiti, mpaka sasa naamini VODA na TIGO ni wezi. Imefikia mahali siwachi au siweki vocha kwenye simu zangu. Maana nikiweka tu zinaingia msg mfululizo na mara nyingine msg hiyohiyo inatumwa hadi mara mbili kwa siku.

Naomba mnisaidie niweze kupata haki yangu.
 
endelea na msimamo huohuo wa kutokuweka vocha kwani utawakomesha...ikishindikana kawaloge kwa mzee manyaunyau
 
bongo kuna haki, mbona wengine tunafanyiwa zaiidi ya hayo tumetulia faza, we kausha mpaka 2015 chini ya chadema
 
Mkuu mimi leo nimeweka salio la 500 voda nikajaribu kujiunga nikawa napewa ujumbe et sina salio nikajaribu kucheck salio et ni zero daaaah huu wizi wa mitandao ya huduma za simu ni noma kaka
 
Katika sms utakayopokea wakati umeweka vocha reply kwa neno. ONDOA utakuwa umetoka kwenye makato. Hata mm nilishakutana na tatizo hilo

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Katika sms utakayopokea wakati umeweka vocha reply kwa neno. ONDOA utakuwa umetoka kwenye makato. Hata mm nilishakutana na tatizo hilo

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

ha ha ha...haya ndugu jamaa anaeza fanikiwa labda.
 
Back
Top Bottom