Mtafiti77
JF-Expert Member
- Oct 31, 2011
- 1,842
- 2,272
Mimi ni mteja wa kampuni mbili za simu; tigo na vodacom. Cha ajabu mitandao hii imekuwa na tabia ya kuniibia pesa kwa hila. Walianza vodacom wakishirikiana na kampuni ya pushmobile. Kupitia huduma waliyoiita burdani wamekuwa wakinitumia msg za ajabu pengine wakidhani kwangu ni burdan kumbe hapana. Kila wakinitumia hukata kiasi cha sh. 150/=. Kwa sasa hao wazee wa burdan wamestop wamezua huduma iitwayo ''mwananchi'', sijui kama inaamaanisha gazeti au la! Nao pia wamekuwa wakinitumia taarifa kwenye line ya tigo na voda. Nao pia hukata 150/= kwa meseji.
Napenda kuwataarifu wanajamii, nipo timamu wala si mlevi; mimi sijawahi kujiunga kwa namna yoyote ile na huduma hizi.Labda mtu anisaidie huenda kuna mtego makampuni haya yameweka labda wakati napokea simu zangu pengine ndiyo niwe nimejiunga au vinginginevyo! Nikijaribu kuwapigia huduma kwa wateja sipati msaada hasa vodacom, tigo huwa nawapigia huduma kwa wateja bila mafanikio. Simu zangu hazishikwi na mtu yeyote! Kwakweli mpaka ntakaposhawishika kwa maelezo thabiti, mpaka sasa naamini VODA na TIGO ni wezi. Imefikia mahali siwachi au siweki vocha kwenye simu zangu. Maana nikiweka tu zinaingia msg mfululizo na mara nyingine msg hiyohiyo inatumwa hadi mara mbili kwa siku.
Naomba mnisaidie niweze kupata haki yangu.