Je, haki itatendeka kwenye ajira hii ya NEC na kura zetu zitapona?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,342
6,468
Tume ya uchaguzi (NEC) imetangaza ajira za aina tatu kwenye gazeti la Daily News 30/09/2010. Nafasi hizi ni ‘karani mwongozaji’, ‘msimamizi’, na ‘msimamizi msaidizi’ kwa manispaa ya Kinondoni. Baadhi ya majukumu ya msimamizi ni kuhesabu kura na kupokea vifaa vya kupigia kura. Haya majukumu mawili ni muhimu sana katika kufanya uchaguzi uwe huru na haki. Baadhi ya sifa ni kuwa mwadilifu na mtiifu. Wasiwasi wangu ni namna ya kuzijua sifa hizi na hasa utii na maana yake halisi – ni kufuata/ kufanya kile unachoambiwa bila kuuliza? Tarehe ya mwisho 08/10/2010.

Hivi kazi hizi zimetangazwa nchi nzima? Kama hapana, ni kwa nini Manispaa ya Kinondoni tu? Je, hizo manispaa nyingine wamewapataje? Je, hawajaandaliwa watu tayari kwa kazi hizi ili wachakachue matokeo?
 
hivi ni wapi wanatuma kama una uhitaji? tangazo liko wapi rasmi... mbona kimya kimya hivi?
 
Wewe pendekeza namna bora ya kuutambua utii...sio kulalama hapa...
 
Back
Top Bottom