Je haiwezekani kuwa na huduma huru za reli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je haiwezekani kuwa na huduma huru za reli?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Laigwanan76, Dec 20, 2011.

 1. Laigwanan76

  Laigwanan76 JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Huwa nakaa najiuliza lakini sipati majibu ya moja kwa moja.Je ubinafsi wa viongozi wetu au hatuna uwezo na utashi wa kushughulikia matatizo yetu kimizania.

  Huduma ya reli ni kama imekufa nchini,ambayo nadhani ilikuwa ikihudumia mamilioni ya watu kwa gharama nafuu.

  Je,huduma hii haiwezi kuwa huru,Zikawepo kampuni kadhaa ambazo zinatoa huduma hii,kusafirisha mizigo na abiria,lakini zinatumia kwa pamoja miondo mbinu iliyowekwa na serikali,na kukawa na kampuni nyinginezo kwa ajili ya kuhudumia usalama wa miondo mbinu na uendelezaji wake?

  Kampuni hizi zikatoa huduma bora kwa wateja wake kulingana na uwezo wa wateja, katika daraja tofauti.Serikali ikabaki kutunga *sera na kusimamia mazingira ya usawa kwenye ushindani .

  Kuna faida nyingi katika hili ikiwa tu kuna nia ya dhati kuhudumia wananchi na kukuza uchumi wa nchi. Kwa mfano leo hii,kanda ya ziwa *na mikoa mbali na bandari kuna upungufu wa bidhaa nyingi zinazotumika katika maisha ya kila siku ,kuanzia baadhi ya vyakula mpaka bidhaa kama mafuta,hivyo kufanya ziwe ghali sana. Hii kwa kiasi kikubwa natumaini inachangiwa na gharama za usafirishaji ambazo usafiri wa reli ungeweza kupunguza na wakati huo huo kupunguza uharibifu katika barabara zetu za" kichinachina *za AFRICAN grade"

  Kwa mfano mwingine,kampuni moja ya Cement hapa TZ inaagiza makaa ya mawe Msumbiji,ingawa wanadai ni bora kuliko ya hapa,lakini kwa taarifa za karibuni makaa yetu ni bora saana.Nachelea kuamini wanjustify hii kwakuwa ni rahisi kusafirisha makaa haya kutoka Msumbiji kuliko kutoka Mchuchuma kutokana na miundo mbinu.Hapa kahela ketu kadogo kakigeni nako kanatoka kwa bidhaa tuliyonayo......?

  "I think it's high time wenye kufanya maamuzi ya mustakabali wa taifa hilo wafanye hivyo unless tutaendelea kuamini hawafikiri kwa vicha vyao ila kwa........................."kama *Mstahiki Meya mmoja kutoka katika moja ya majiji ya nchi alivyopata kusema!

  Poleni kwa urefu wa gazeti na lack of composition.........
   
 2. Laigwanan76

  Laigwanan76 JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Duu wazee naona huu uzi haujagusa hisia za watu kabisa
   
Loading...