bm21
JF-Expert Member
- May 12, 2008
- 774
- 33
Gamba la Nyoka mkuu heshima mbele. Ninavyoelewa mimi taarifa zilizoandikwa hapo haziwezi kuhatarisha usalama wa Taifa kwani hakuna kitu sisi tunachokiiti siri ambacho hakifahamiki na wazungu kwani silaha zenyewe tunanunua kwao halafu kwa umaskini wetu World Bank na IMF huwa wanadodosa juu yA MILITARY SPENDING YETU KABLA HAWAJATUFADHILI MIKOPO; tunalazimika kuwapa taarifa za majeshi yetu!! Taarifa za jeshi letu sio siri tena na ndio maana hata wewe umeweza kuzipata!!! Usalama wa Taifa letu ni jukumu letu mimi na wewe kuwatokomeza hawa mafisadi kwani fisadi kama Rostam anaweza kuliangamiza Taifa letu kwa jinsi alivyowaweka mifukoni viongozi wa nchi yetu!!
Mkuu hapa nadhani hupo sahihi. Tatizo letu sio mataifa makubwa kwani hata siku moja hatuwezi kushindana nao wala kupigana nao. Tatizo hapa ni hawa wenzetu wadogo wadogo wakijua mambo yetu ya ndani ni hatari. Mfano tukitaka kuichapa mfano Kenya au Uganda hivi kama inajua strength ya jeshi letu inaweza kutushinda kwa kujiandaa vilivyo. Natumaini hata hao mataifa makubwa yanayolazimika kujua silaha tulizonao wana miiko yao hawawezi kupablishi details kama hizi