Je, Gazeti la The Guardian nchini linaunga mkono Malawi dhidi ya Tanzania kwenye mgogoro wa mpaka?

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
IMG_0194.JPG

Katika taarifa yake ya Julia 12, 2017, The Guardian lilielezea kwanza na kwa kirefu msimamo wa Malawi katika mgogoro wa mpaka dhidi ya Tanzania, huku likitoa msimamo wa Tanzania kwa lugha ambayo inaonyesha kuwa nchi inapinga tu.

Hata hivyo, kwenye ukurasa wa ndani, nimeshangaa kukuta kibonzo kinaonyesha msuluhishi akielekea kuipa Malawi haki ya umiliki wa Ziwa Nyasa. Watalaamu wa vibonzo mtusaidie, huyo mwandishi alimaanisha nini?
 
Lakini kwa nini aanguke? Huyo ni msuluhishi. Halafu mbaya ameshikilia kitu kwenye mkono mmoja. Mchoraji alitaka kutuambia nini lakini?
mchoraji aliwahi kuchora akasahau maana ya anachokichora.
hicho kibonzo hakionyeshi faida kwa yoyote. labda kama kilimaanisha kupatana ndio option pekee
 
Kwahio unataka lifungiwe au ? Uhuru wa habari upo wapi ?
 
Tena cha ajabu, wakati pande mbili zinazovutana zimenuna, yeye anatabasamu. Hii ina maana gani?
 
Kwahio unataka lifungiwe au ? Uhuru wa habari upo wapi ?
No sijafika huko hata kidogo. Ni muhimu vyombo vya habari yenye ushawishi visichezee maslahi ya Taifa kwa lingo la kutoka kuuza tu gazeti. Hii ni kwa sababu kwa sasa mkutano wa usuluhishi unaendelea SA tangu jana na mnajua magazeti sasa Hivi yanasomwa kimtandao na ni lazima hiyo panel ya wasuluhishi itataka kujua reactions ya watanzania na wamalawi juu ya usuluhishi unaoendelea. Hivi anakutamsuluhishi anakuta Gazeti kubwa kabisa kwa wasomi nchini ndiyo linaonyesha doubts dhidi ya haki ya Tanzania kwenye mgogoro huo. Wao watanzania kuwa huo ndio msimamo wa watanzania. Tujihadhari sana.
 
Inawezekana mhariri ni wa Malawi

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
Hapo ujue litakuwa ni tatizo kubwa sana kwa usalama wa nchi yetu. Ni wahariri wa namna hiyo ndiyo wanatupeleka peleka tu bila hata kuangalia maslahi ya Taifa letu.
Mimi the Guardian ndiyo gazeti langu namba moja nchini ninalopenda lakini na Kirk wazi kuwa kwa hili wamechemka bila kupepesa macho.
 
Sishangai Linamilikiwa na Wachaga

CHADEMA = WACHAGA
Siku zote akili yako haiwezi kung'amua mambo yanayohitaji akili. Kwako wewe umeaminishwa ukabila tu... Wapumbavu kama nyie ndio mnaosababisha nchi zinaingia kwenye machafuko yasiyo na u lazima! Uchaga na Chadema wameingiaje hapo?
Kama huelewi mantiki ya katuni kwa kuangalia picha na maandishi yake, ni vema kukaa kimya ukaacha watu wenye ubongo mzuri waendelee na mjadala.
 
Jamani kwa nini mnajadili negatively kwenye hiyo katuni?
Kwangu Mimi hiyo katuni inatoa tahadhari kubwa sana kwa Mataifa haya mawili. Wenye akili zisizoelewa sanaa wanakimbilia kulisakama gazeti na wengine kwenda mbali zaidi na kuhusisha Kabila la mmiliki wake na upumbavu wao wa ukabila na ujinga wao kwenye ufuasi wa vyama.
Katuni inonyesha mvutano huu wa kugombania mpaka kati ya Tanzania na Malawi unaweza kuwavutia mafisi na wasioyatakia mema mataifa haya mawili. Badala ya kuwaweka pamoja na kutafuta ufumbuzi, manyang'au haya yanaweza kutumia fursa ya mgogoro huu kupalilia utengano zaidi kati ya mataifa haya mawili yanayoingilia kisiasa na kijamii kwa miaka mingi...
Kuna watu wanautazama mgogoro huu kama fursa ya kiuchumi kwao kwa kuingiza ajenda zenye manufaa na faida kwao.
Zaidi wenye uwezo mzuri wa kufikiri kwa kina wataelewa kitakachofuata!
Hii katuni ilipaswa ikae ukurasa wa mbele ili wahusika na wafanya maamuzi katika nchi hizi waweze kuipata tahadhari hii!
Kwangu Mimi gazeti limetimiza wajibu wake...
 
Wewe hauoni mikono? Kwani kulia kwa msuluhishi ameshikilia kitu gani hicho? Na mkono wake wa kushoto ameshikilia nini?
We Jamaa sijui hujanywa chain...sasa kama ni right hand ashikie mkasi mkono gan...halafu mbona nani naweza sema kwa kidole cha kushoto anaonyesha mmiliki halali ni Tanzania...acha uchonganishi

Sent from my TECNO DP7CPRO using JamiiForums mobile app
 
Jamani kwa nini mnajadili negatively kwenye hiyo katuni?
Kwangu Mimi hiyo katuni inatoa tahadhari kubwa sana kwa Mataifa haya mawili. Wenye akili zisizoelewa sanaa wanakimbilia kulisakama gazeti na wengine kwenda mbali zaidi na kuhusisha Kabila la mmiliki wake na upumbavu wao wa ukabila na ujinga wao kwenye ufuasi wa vyama.
Katuni inonyesha mvutano huu wa kugombania mpaka kati ya Tanzania na Malawi unaweza kuwavutia mafisi na wasioyatakia mema mataifa haya mawili. Badala ya kuwaweka pamoja na kutafuta ufumbuzi, manyang'au haya yanaweza kutumia fursa ya mgogoro huu kupalilia utengano zaidi kati ya mataifa haya mawili yanayoingilia kisiasa na kijamii kwa miaka mingi...
Kuna watu wanautazama mgogoro huu kama fursa ya kiuchumi kwao kwa kuingiza ajenda zenye manufaa na faida kwao.
Zaidi wenye uwezo mzuri wa kufikiri kwa kina wataelewa kitakachofuata!
Hii katuni ilipaswa ikae ukurasa wa mbele ili wahusika na wafanya maamuzi katika nchi hizi waweze kuipata tahadhari hii!
Kwangu Mimi gazeti limetimiza wajibu wake...
Unaelewa kweli wewe kinachoendelea Afrika Kusini tangu jana? Sasa mambo ya kutukana yanatoka wapi ndugu. Mimi nimefurahi ulivyosema kuwa hiyo matusi inatoa tahadhari, huo hao ni mtazamo wako lakini usijisahau ukadhani Wewe ndiye umepatia ama kwamba wengine watakiona kibonzo hicho kwa jinsi ulivyokiona.
 
We Jamaa sijui hujanywa chain...sasa kama ni right hand ashikie mkasi mkono gan...halafu mbona nani naweza sema kwa kidole cha kushoto anaonyesha mmiliki halali ni Tanzania...acha uchonganishi

Sent from my TECNO DP7CPRO using JamiiForums mobile app
Nashukuru kwa mtazamo wako lakini ukweli utabaki palepale kuwa, The Guardian halijatufanyia haki hata kidogo.
 
Hivyo vi-Malawi vinajifanya vijuaji sana, nimekuwa nikifuatilia vinajidai kujiapiza kuwa hakuna kipindi chochote cha kinachodai ardhi (maji) kitakachotolewa.
 
Nashukuru kwa mtazamo wako lakini ukweli utabaki palepale kuwa, The Guardian halijatufanyia haki hata kidogo.
Ila boss lazima ujue ukiweka uzalendo pembeni..haki sio sheria..Tunaweza kua na haki ila mikataba ya kikoloni inatukaba..halafu Katuni ni fasihi andishi huwezi I judge hivyo

Sent from my TECNO DP7CPRO using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom