Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 235
Baada ya kuelezea kidogo jinsi ya kutrace email na mambo mengine watu wanataka kujua jinsi ya kuficha ip address zao , wengine wameuliza kama forum wanazotembelea ni salama au la , wengine wanaogopa kukanyaga hizi forum kutokana na usalama .
Labda tuambiane ukweli kila forum inatakiwa iwe na sheria na kanuni zake , wakati unajisajili tafadhali soma hizo sheria na kanuni zinasema nini katika usalama wa mtu uhuru na mambo yake mengine pindi anapotuma au kuchangia kitu Fulani .
Ubaya ni kwamba forum nyingi zinatumia sheria na kanuni za nchi za ulaya na asia kwa sababu zimetengenezwa na watu wa huko mara nyingi au mtu amenunua huko kwa njia ya mtandao au kwa njia zingine kwahiyo unakuta vifungu vinavyoelezea ni vya nchi hizo husika .
Sasa sijaweza kujua kama mimi niko hapa , nimechangia kitu kikaleta balaa inapofikia wakati wa kutolewa kumbukumbu zao zitatumika sheria za wapi au itafanyika utaratibu gain kwa sababu hapa Tanzania sheria mtandao ndio hii ambayo watu wanahepa kuongelea mara kwa mara .
Kwa vyovyote vile tunapoongelea usalama wa forum na wanachama huu ni uhusiano kati ya mwenye kumiliki au kuendesha forum hiyo na wanachama wa forum hiyo , kuna forums ambazo kuna wengi zaidi wenye maamuzi ya kuweza kuangalia nani yuko wapi na kutoa siri hizi kwa watu wengine wasio husika .
Kwa leo tutaangalia mfano wa phpbb , kumbuka kuna programu nyingi zinazotumika katika kuendesha hizi forum mimi nimeamua kutumia phpbb kama mfano utaweza kuona jinsi mtu anavyoweza kuwa na taarifa zako chache tu .
ANGALIA ATTACHEMENT KWA MAELEZO ZAIDI