Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 54
na Ramadhani Siwayombe, Arusha
MGOGORO sehemu itakapozikwa maiti ya mtoto wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Felix Mrema, umechukua sura mpya baada ya mbunge huyo kudaiwa kuondoka hapa nchini kwa kificho na kwenda nchini Marekani kwa lengo la kufanya mazishi nchini humo.
Habari zilizopatikana jijini hapa, jana na kuthibitishwa na ndugu wa marehemu walioko nchini Marekani zinaeleza kuwa mbunge huyo hivi sasa yupo nchini huko kwa lengo la kufanya maziko ya mwanae huko bila kumshirikisha mkewe wa ndoa, Milcah Mrema, aliyeko hapa nchini.
Kutokana na mgogoro uliopo wa wazazi juu ya sehemu atakayozikiwa mwanao, Angel Mrema, 34, maiti imefikisha siku 20, bila kuzikwa.
Akiongea na Tanzania Daima mara baada ya kupata taarifa hizo mama mzazi wa marehemu, Milcah Mrema, alisema nguvu ya fedha aliyonayo mbunge huyo ndiyo inayomnyanyasa na kumkosesha haki zake za msingi.
''Mimi ni mzazi mwenzie ambaye wote kwa pamoja tumefiwa na mtoto wetu na tuna machungu kwa hilo lakini mwenzangu kaamua kuondoka bila hata kuniaga na kwenda huko kufanya taratibu za mazishi bila kunishirikisha.'' Alieleza mama huyo kwa machungu.
Aidha mama mzazi wa marehemu akiongea kwa masikitiko mjini Arusha alisema, kinachomuuma ni kusikia kuwa mazishi yanayotaka kufanyika huko ni kwa njia ya kuchoma moto mwili wa marehemu kutokana na nafasi za kupata makaburi kutokuwepo ambapo ni kinyume na utaratibu wa dini yao Kikristo.
Amesema kuwa licha ya kwenda kinyume na misingi hiyo ya mazishi ya dini pia haki ya kuwa anafanya maombi dhidi ya mtoto wake kwa kutembelea kaburi na kuweka maua inakiukwa kutokana na maamuzi yanayotaka kufanywa na mumewe.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Marekani katika jimbo la Los Angeles ambako ndiko mwili huo wa marehemu uliko mama mkubwa wa marehemu, Muthike Phyllis Porter, amethibitisha kufika huko kwa mbunge huyo na kuanza taratibu za mazishi.
Muthike ambaye anaishi katika Jimbo la Washington DC nchini Marekani alienda Los Angeles kwa ajili ya kufanya taratibu za kusafirisha mwili huo kuuleta hapa nchini kwa maelekezo ya ndugu yake lakini kufika huko kwa Felix Mrema kumesimamisha mipango hiyo.
Marehemu Angela Mrema, mtoto wa Mbunge wa Arusha Mjini, Felix Mrema, alifariki dunia Desemba 17 mwaka jana nchini Marekani baada ya kupata ajali ya gari Desemba 7; ajali iliyosababisha kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia mguu na wakati akiwa katika matibabu hayo, alifariki dunia akiwa katika chumba cha upasuaji.
Mara baada ya kupatikana kwa taarifa za kifo hicho familia ya marehemu iliyopo mjini Arusha wakiwemo baba mzazi wa Marehemu, Felix Mrema, na mkewe Milcah ambaye kwa sasa haishi na mumewe huyo baada ya mbunge huyo kuwa na mke mwingine, kulizuka mvutano wa sehemu utakapozikwa mwili huo.
Katika mgogoro huo, mama mzazi wa marehemu anataka mazishi ya mwili wa mtoto wao uzikwe hapa hapa Arusha, huku baba, Felix Mrema, akitaka shughuli yote ya mazishi kufanyika huko Marekani.
Jitihada za kumpata mbunge huyo kwa njia ya simu ili azungumzie hatua iliyofikiwa juu ya taratibu za mazishi haikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila majibu.