Je, faini za magari haya ni mradi halali wa jiji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, faini za magari haya ni mradi halali wa jiji?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, Jan 7, 2009.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Maegesho ya magari jijini Dar es Salaam siyo mengi sana. Na kwa jiji lilivyo hata kujua wapi haparuhusiwi au panaruhusiwa kuegesha gari siyo rahisi. Cha kushangaza utakuta mgambo wa jiji wakiyavuta magari, ambayo wanadai yaliegeshwa maeneo yasiyoruhusiwa. Na mwenye gari anapoenda kuchukua gari lake, huambiwa alipie fani kiasi fulani (nasikia hadi Sh80,000 au zaidi).

  Kwa mawazo yangu, kwanza sehemu za kuegesha magari zingefahamika na sehemu zisizoruhusiwa kuegesha pia zingefamika (ziwekwe alama mfano: Hairuhusiwi kuegesha au Egesha gari hapa (Parking Prohibited/Parking Area). Kisha, anayekaidi maagizo hayo achukuliwe hatua - alipe faini.

  Lakini ninachoona kinaendelea jijini, siafiki kabisa. Naona kama ni mradi wa jiji kwa vile faini zinaongeza pato. Je, kuendelea kulipa faini kwa namna hii kusiko lenga kuongeza au kuboresha sehemu za maegesho ya magari siyo aina fulani ya ufisadi jijini Dar es Salaam?
   
Loading...